MESHACK ABEL MWAMKINA
IMEANDIKWA NA ABDUL SUDI,MBEYA
meshack abel akimdhibiti mshambuliaji wa Gor Mahia
Alizaliwa Mbeya,eneo la Ghana na kusoma
katika shule ya msingi Mbata na baadae sekondari akasoma Sangu.
Kama ilivyo kwa watoto wengi wa Tanzania Meshack Abel alianza kucheza mpira toka akiwa mdogo sana,kwanza jirani na kwao,kisha kidogo kidogo
kipaji chake kilipoanza kuonekana akawa anachukuliwa na wenzake na kwenda
kucheza mbali kidogo na nyumbani kwao.huko alikutana na watoto wengi wenye
vipaji kama vyake na ikawa rahisi kumshawishi na kwenda kuingia katika ligi za
watoto zilizokua zikifanyika katika sehemu iliyojulikana kama kiwanja
ngoma,kwake ilikua ni rahisi kwani kaka yake aliyekua akiitwa Reuben au maarufu
kama ‘masox’alikua ndie mchezaji maarufu zaidi ya watoto wengi wa eneo
lile,hivyo alikua kama kamsafishia njia,lakini Meshack hakumuangusha kaka yake
kwani nae akatokea kua mzuri zaidi ya
kaka yake.
Hapo Kiwanja ngoma aliichezea kwanza timu
iliyoitwa Saitama na baadae Snow White na alikutana na watoto wengi waliokua na
viwango vya juu sana na ambao karibu wote baadae walikuja kucheza katika ligi
kuu ya Tanzania.Mbali na kaka yake Reuben aliekuja chezea AFC ya
Arusha,alikutana na kina Jaafar Muhoza,Vicent Barnabas,Yona Ndabila,Shaaban
Mtupa,Mbega Daffa,Misengo Magai,David Naftari,Bantu Admin,na wengine wengi.wakati
huo alikua akicheza nafasi ya kiungo,ambayo mwenyewe anasema alikua anaimudu
sana.
Meshack alitoka moja kwa moja kiwanja ngoma
na kuchukuliwa na timu ya AFC iliyokua ikicheza ligi kuu ya Tanzania,na huko
alicheza katika kiwango cha juu sana kiasi kocha aliyekua akiifundisha Mtibwa
wakati huo Sunday Kayuni alimchukua na kumuhamishia katika timu ya Mtibwa,na ni
yeye Sunday Kayuni aliyembadilisha namba kutoka kiungo na kumrudisha nyuma
namba ambayo anacheza hadi leo.Baada ya kucheza Mtibwa kwa mafanikio
viongozi wa Simba wakamfuata na kumtaka ajiunge na timu yao,ndipo alipojiunga
na Simba,Alipokua Simba alichaguliwa na Maximo katika timu ya taifa.alikaa
Simba kwa muda kisha akahamia Kenya katika timu ya Bandari ambayo ndio yupo
hadi sasa.
MESHACK ABEL (WA PILI KULIA)AKIWA NA KIKOSI CHA BANDARI YA KENYA
Nilipomuuliza tofauti ya mpira wa
Tanzania na Kenya akanambia “Unajua wenzetu huku wanajali sana kazi zao,huwezi
kukuta mchezaji anachelewa mazoezini bila sababu maalum,na pia wachezaji wa
huku wanamsikiliza sana kocha tofat na kwetu wachezaji wanakua juu ya kocha,na
hata upangaji wa timu huku anaachiwa kocha moja kwa moja lakini Tanzania kocha
anakua chini ya viongozi na wao ndio wanapanga timu na kujidai kama wanamshauri
kocha,kumbe wanamlazimisha wanachotaka,mfano timu kama Simba ina bahati sana ya
kupata makocha wazuri mno wa kiwango cha juu,lakini wanaingiliwa na viongozi na
wafadhili hadi wanachanganyikiwa,mimi binafsi ukiniuliza kocha niliyekua
namkubali sana Simba na ikaniuma sana aliopoondoka nitakwambia ni Benziski,Yule
jamaa alikua anajua sana niliumia sana alipoondoka”aliongeza Meshack ambae anakiri
kuwa kwake kama mtanzania yeyote mechi kubwa sana alizowahi kucheza hapa
Tanzania ni kati ya Simba walipocheza na Yanga “mechi ya Simba na Yanga ndio
mechi yangu kubwa hadi sasa kuicheza kwani ingawa inakua ni ya dakika 90 lakini
inachukua muda mrefu sana kuzungumziwa na utayarishwa kiasi mnakua mnaisubiri
kwa hamu sana….”alinambia Meshack

