“ THE TALENTED”
Mmoja kati ya wachezaji wenye vipaji
halisi hapa Tanzania ni Uhuru Selemani,kwani pamoja na misuko suko ya majeruhi
iliyokua ikimkabili lakini kila akiingia uwanjani anaonyesha kiwango kile kile
alichokua nacho kabla ya kuumia.Na sasa hivi ,yupo vizuri zaidi ya alivyokua misimu iliyopita.
“namshukuru Mungu sasa hivi nipo salama,sina tatizo tena na naomba uzima
nitaonyesha kiwango kikubwa zaidi ya nilichoonyesha kabla”alinambia Uhuru ambae
kwa sasa yupo Coastal Union akitokea klabu ya SImba aliyokua nayo msimu
uliopita. “unajua ukiwa majeruhi wa mara kwa mara hata wewe mwenyewe
unachanganyikiwa,unakua hujiamini,uoga wa kuumia unakufanya usicheze kwa uhuru
unaoutaka,lakini kwa sasa niko vizuri mno na naamini nitaonyesha kiwango changu
halisi”
Uhuru ana uwezo wa kucheza namba nyingi
uwanjani,kwani pamoja na mara kwa mara kuchezeshwa kama kiungo wa pembeni
lakini ana uwezo wa kusimama kama mshambuliaji na hata kucheza kama kiungo wa juu.na kama lilivyo
jina lake yupo huru sana akiwa na mpira kiasi ana uwezo wa kupiga chenga huku
anakwenda mbele na pia ana uwezo wa kupiga miguu yote hivyo inakua ni ngmu sana
kwa mabeki kumkaba akiwa na mpira,wanakuwa hawajui ataufanya nini mpira,na hata
ukitazama magoli anayofunga ni ya uhakika si ya kubahatisha,kwa vile ana kipaji
halisi.ni wachezaji wachache sana wenye uwezo wa kkupiga mashuti huku
wanakimbia,lakini Uhuru anafanya hivyo mara kwa mara…
Uhuru Selemani alizaliwa mkoani Mbeya
katika wilaya ya Mbarali na alianza elimu yake ya awali katika shule ya msingi Mbarali na kuja kumalizia Kawe Dar es
salaam “toka nikiwa shule ya msingi nilipenda kucheza mpira,kiasi nilipokua
mkubwa kidogo nikajiunga na wenzangu katika timu ya Ibara kids,pale tumecheza
sana kisha baadae nikachukuliwa na rujewa kids zote za Mbeya na hata
nilipohamia Dar moja kwa moja nikajiunga na ukwamani kids yak awe,,na huko
tukawa tunafanya vitu vikubwa kiasi tukapata mashabiki wengi sana….unajua
nimecheza mashindano ya muungano Mufindi nikiwa na umri mdogo sana lakini nilikubalika
kwa vile kiwango changu kilikua ni cha uhakika”
Uhuru amewahi kuchezea timu kadhaa ikiwemo
Mtibwa,Coast,Azama ,na Simba ana uzoefu
wa kucheza katika hali yoyote
“Ninashukuru nimeanza kucheza mpira wa ushindani nikiwa mdogo sana hilo limenikomaza
na kuweza kupambana na changamoto za kila aina,kila timu unayokwenda unakuta
ina mifumo yake,tokay a uchezaji hadi ufundishaji,hivyo nimepitia mambo mengi
sana sasa hvi nishakua mzoefu wa fitna za soka”alinielezea. “Nafurahia sana
maisha ndani ya timu yangu ya Coastal Union,kwani hakuna mazengwe ya
kutengenezeana,hapa mtu unacheza kutokana na kiwango chako,tofauti na inavyokua
kwa timu hizo zinazoonekana ni kongwe hapa Tanzania,kule mwenye sauti ya mwisho
nani acheze na nani asicheze si kocha,ni watu tofauti kabisa wenye nguvu za
ajabu katika hizo timu,ndio maana utashangaa kila siku wanaacha wachezaji
wazuri na kusajili vichekesho,nimepita huko najua naloongea,unafanya mazoezi
vizuri,kocha anakufurahia na kukusifu na kukupa matumaini unajua mechi inayokuja
unacheza lakini baadae ikitajwa list unakua haupo,kisha unaanza kusikia
rumours,kua kuna kiongozi pengine hakupendi au hataki ucheze…unaweza hata
kuzushiwa sababu za ajabu…huna nidhamu au lolote na itokee bahati mbaya
ukakosea siku uliyopangwa mashabiki wale wale wa timu yako ndio wanakua wa
kwanza kukupigia kelele na kumlazimisha kocha akubadili…siwalaumu kwani najua
wanakua tayari wameshalishwa sumu”aliongea Uhuru “lakini kwa timu nyingine hali
ni tofauti,presha inakua ndogo ndio maana hata mchezaji unakua na amani na
unafanya vizuri.
Uhuru amechaguliwa mara kadhaa kuichezea
timu ya Taifa,na mechi ambayo kila mtu anaikumbuka ni siku Tanzania walipocheza
na Brazil “kila mtu duniani anatamani kucheza na Brazil,nashukuru mumngu
nilipata nafasi ya kucheza na wachezaji bora kabisa duniani,mara nyingi
unawaona katika tv lakini nimebahatika kucheza nao…fikiria unacheza na mchezaji
unaempenda kama Robinho,unakabwa na mchezaji kama Dani Alves,hiyo ni kumbukumbu
nitakayobaki nayo hadi nakufa maana si wote wenye bahati kama yangu”
Kwa sasa Uhuru amesajiliwa na timu ya
Coastal Union ya Tanga akitokea timu ya Simba.na kwa matayarisho aliyoyafanya
ana uhakika wa kucheza vizuri zaidi
msimu huu….tuko pamoja HOME BOY……












