Mchezo
wa marudiano kati ya Yanga na Al Ahly ya Misri umepangwa kufanyika katika
uwanja wa Harras el Hadoud uliopo Alexandria
Misri siku ya jumapili, badala ya jijini Cairo.
Timu ya soka ya Taifa Stars ya
Tanzania, wametoka sare na Brave Warriors ya Namibia kwa kufungana goli moja
kwa moja katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Simba imezinduka baada ya kuifunga
Ruvu Shooting kwa magoli 3-2, katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Tanzania bara. Hadi mapumiko Simba walikua wakiongoza kwa magoli mawili yote
yakifungwa na Amis Tambwe.