Friday, 21 February 2014

Ni coastal  na mbeya city.

   Mbeya City wana mtihani mwingine leo pale wanapokutana na timu ya Coastal Union ya  Tanga katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania, mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Mkwakwani Tanga na kuonyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Azam Tv.
Tz prisons kamili kuwavaa azam

   Kikosi cha Tz Prisons kipo tayari kupambana na timu ya Azam wikiendi hii katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Azam Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar.

Thursday, 20 February 2014

Anthony matogoro 
Mpiganaji wa mbeya city

 
     Mmoja kati ya wachezaji wanaotamba katika timu ya Mbeya City  ni Anthony Matogoro, Kiungo wa chini  anaekaba toka mwanzo wa mchezo hadi mwisho, ni mpiganaji halisi ambae kila timu inatamani iwe na mchezaji wa aina yake. Ni mrefu na hilo linamsaidia kucheza mipira yote ya juu inayokuja upande wake, ana nguvu pia ana akili kubwa ya kusoma njia za mpira, hivyo anakua na uwezo mzuri wa kukisia uelekeo wa mpira, na kufanya iwe rahisi kukutana nao na kuunasa au kuharibu pale inapobidi.

Sunday, 16 February 2014

Mbeya city walivyopambana na simba

 Mbeya City wamefanikiwa kutoka sare ya goli moja kwa moja na timu ngumu ya Simba iliyocheza kwa kiwango cha juu sana kuonekana hivi karibuni. Katika mchezo huo Simba walionekana kujaribu kumiliki kila idara na kuwafanya Mbeya City muda mwingi kujitahidi  kuharibu mipango ya Simba.