MASHABIKI WA MBEYA CITY WALIVYOSUMBUA ARUSHA
NA ABDUL SUDI.
Kundi la
mashabiki wa timu ya Mbeya City walisafiri kuifata timu yao ilipokwenda Arusha
kupambana na JKT Oljoro,Baada ya kufika Arusha walikutana na wennzao waliokua
wanaishi pale pale na kuanza kusherehekea kabla hata mechi
haijaanza.wakizungumza na Mbeya Maskan’
wamesema wameamua kwa mapenzi yao kwenda mji wowote timu itakapokua ikicheza
ili kuipa sapoti na kuona wenyewe kwa macho yao timu wanayoipenda ikicheza.Mmoja wa mashabiki
hao Ally Makenya “popo”ambae ndie aliyeshughulika na kuwapokea mjini hapo
alisema wanapata faraja sana kuona timu ya nyumbani inafanya vizuri na
haibahatishi hivyo wapo tayari kwa hali na mali kuhakikisha inapata sapoti
kubwa nje ya uwanja na wao wapo tayari kutoa sapoti hiyo.
ALLY MAKENYA AKIHAMASISHA
Muda wote wa
mchezo walikua wakishangilia na kuwafanya wakazi wa Arusha kuwashangaa wanatoa
wapi nguvu hiyo ya kushangilia.akiongelea hilo mkazi wa Arusha Josef Malya
alisema amezoea kwenda kutazama mechi nyingi sana hapo arusha hata zikija timu
kubwa za Yanga na Simba lakini hajawahi kuona
watu wanaoshangilia kwa moyo kama hawa mashabiki wa Mbeya City “hawa
jamaa wanshangilia hata kama wanafanya vibaya tofauti na mashabiki wa Yanga na
Simba ambao mchezaji wao akikosea wanamzomea lakini hawa wanashangilia tu na
kuwapa moyo wachezaji wao,inafurahisha sana”alimalizia Malya.mtu mwingine
aliyekuwepo uwanjani ni mfanyabiashara kutoka Shinyanga Abraham Shija,yeye
anasema hajawahi kuona watu wanafurahia timu yao kama mashabiki wa Mbeya
City,kwani toka mchana kabla kabisa ya mchezo haujaanza tayari walikua
wameiteka mitaa ya Arusha na kuonekana kama burudani mpya mjini hapo “nasikia
jamaa wamesafiri na mpiga ngoma wao toka Mbeya,sijawahi kuona mikoa mingine
ikiiga hata nusu ya hawa jamaa nadhani mpira utaendelea sana hapa Tanzania”alisema
Shija.


katika
mchezo huo Mbeya City walishinda 1-0 na baada ya mchezo kumalizika mashabiki
hao waliingia katikat ya uwanja na kucheza na kuimba kwa muda mrefu sana kwa
furaha.Akiongea baada ya mchezo huo kocha wa timu hiyo alisema "namshukuru Mungu kwa kuweza kutusaidia kushinda mchezo huu,pia nawashukuru sana wachezaji wangu kwa kucheza kama nilivyowaelekeza,na kikubwa kilichotusaidia ni nidhamu kubwa iliyoonyeshwa na wachezaji ndani ya uwanja kwani kwa hali ya kawaida presha waliyokuja nayo JKT baada ya kufungwa ilikua kubwa sana wahezaji wasingetuliza vichwa hali ingekua nyingine,hivyo wachezaji wamefanya kazi kama walivyoelekezwa,pia napenda sana kuwashukuru watu wa Mbeya kwa sapoti wanayozidi kutupa kwani inatupa faraja sana na kujiona tuna deni la kulipa,tunawashukuru sana na tutajitahidi tusiwaangushe"
OYOOOOOOOOO
Nae shabiki aliyesafiri kuifata timu toka Mbeya aliyejitambulisha kwa jina la Maka alisema "kwa muda mrefu Mbeya tunajiamini tuna wachezaji wengi wazuri,na vle vile tunajiamini tunapenda sana mpira,sasa hivi watu wamegundua,unajua miaka ya zamani wakati timu za Tukuyu Stars na Mecco zilipokua juu watu wengi walikua wanahisi zina mapenzi na timu za Yanga na Simba hivyomara nyingi mtu ulikua unajua kuwa mechi hii watafungwa na mechi hii matokeo yanaweza kua tofauti,lakini sasa hivi hawa Mbeya City wanatupa raha sana maana wanakomaa kila mech,hakuna cha Siba wala Yanga,zibaki huko huko na mipira yao ya mdomoni...maana wanavyosifiwa katika magazeti ni tofauti na uhalisia...sisi ndio Mbeya hatutaki sifa ni kazi kwenda mbele"alimalizia huku akiwafata wenzake na kuendelea kucheza.
TUMESHINDA.....