Yanga yanoga
Timu ya Yanga imeweza kuwafunga
Ruvu JKT kwa magoli 4-0 katika mchezo wa upande mmoja ambapo Yanga waliutawala
mchezo huo katika vipindi vyote viwili.
Yanga walipata goli la kwanza mapema
katika kipindi cha kwanza lililofungwa
na Mrisho Ngasa baada ya kupata pasi toka kwa Domayo na akawahadaa mabeki wa Yanga wakidhani anataka kutoa pasi ndipo alipopiga shuti kali lililomshinda kipa
wa JKT na kuingia golini.
JKT hawakuonyesha kutulia na mabeki wake
walikua kila mara wakijichanganya na kuwafanya Yanga wazidi kutawala mchezo, goli
la pili lilifungwa tena na Mrisho Ngasa baada ya mpira uliorushwa na Mbuyu
Twite kuwapita mabeki wa JKT na ukadunda na kumkuta Ngasa aliyepiga kichwa na
kuandika goli la pili.
JKT walicheza bila ya maelewano na hasa
viungo wao waliokua wakipoteza mipira mara kwa mara na kuwafanya viungo wa
Yanga kua na kazi rahisi ya kusambaza mipira kila upande.
Yanga walipata goli la tatu kupitia kwa beki wake wa kushoto Oscar
Joshua baada ya kona iliyopigwa na Ngasa kuokolewa kizembe na mabeki wa JKT na
mpira kumkuta Joshua aliyepiga shuti zuri la mguu wa kushoto na kuandika goli
la tatu
Waliendelea kushambulia na mshambuliaji
wake Jerry Tegete alikosa nafasi tatu za wazi kufunga magoli na baadae
kufanikiwa kufunga baada ya kuukuta mpira uliowapita mabeki wa JKT na kuandika
goli la nne.hadi mpira unamalizika Yanga wakaondoka na ushindi wa magoli manne
kwa bila.










