Saturday, 20 September 2014

KARIBUNI MBEYA CITY INAWASUBIRI

KARIBUNI
MBEYA CITY INAWASUBIRI
        Msimu mpya wa ligi umefika, Mbeya City inaanzia pale pale ilipoishia msimu uliokwisha.
Ilishika nafasi ya tatu, hakuna aliyetegemea hilo,  lakini liliwezekana,  na sasa hivi inatarajia kwenda juu zaidi. Ni kazi ngumu,  ukichukulia timu zote zitakua zinaipania Mbeya City, kwani wanajua wakifanya makosa muziki wa City ni mkubwa , wataadhirika.

Friday, 19 September 2014

Beno kakolanya
    TZ PRISONS ONE

Baada ya katikati ya msimu uliopita kuondokewa  na aliyekua kipa nambari moja wa Tz Prisons, Wilbert Mweta, mashabiki wa soka walitegemea timu hiyo itashuka daraja, kwani katika mzunguuko wa kwanza, ilikua ipo chini kabisa mwa msimamo wa ligi, hivyo kuondoka tena kwa kipa tegemeo kuliwapa wasiwasi wengi.

Tuesday, 16 September 2014

 Ivo mapunda
KIPA ASIYECHUJA TANZANIA

   
Ukiongelea makipa bora kabisa waliowahi kutokea hapa nchini na bado wanatamba huwezi kuacha kumtaja Ivo Mapunda, pamoja na kua alianza kucheza mpira muda mrefu, lakini hadi sasa ubora wake unazidi kuongezeka.  Ana uwezo wa kucheza mipira ya aina yote, ya juu na ya chini, pia umbo lake kubwa linamsaidia hata katika ile mipira ya kupambana na ya krosi