Saturday, 5 October 2013

MBEYACITY YAICHAPA OLJORO  2-1

                                                mbeya city
Timu  ya Mbeya City imefanikiwa kuifunga timu ya JKT Oljoro ya Arusha kwa magoli mawili kwa moja katika mchezo mkali na mzuri uliochezwa katika uwanja wa sheikh Amri Abeid Arusha.City ndio waliokuwa  wa kwanza kupata bao lililofungwa na mshambuliaji hatari Mwagane Yeya baaada ya krosi safi iliyopigwa toka kushoto mwa uwanja na mpira ukamkuta Paul Nonga aliyepiga shuti kali lililomshinda kipa wa Oljoro na mpira ukawa unaelekea golini  na ndipo mwagane akaumalizia na kuandika goli la kwanza.City walikitawala kipindi cha kwanza na hadi mapumziko goli likawa hilo moja.kipindi cha pili Oljoro waliingia kwa nguvu na kufanya mashambulizi mengi kuelekea kwa City,na uhodari wa mabeki wa City wakiongozwa na Yohana Morris na kipa Baruan walikua makini na kuweza kkuzuia mashambulizi hayo.City wallipata bao la pili kwa counter attack baada ya Oljoro kufanya shambulizi kali golini mwa City na ndipo kipa wa City Baruan alipodaka akapiga mpira mrefu uiomkuta Peter Mapunda aliyekua katikati ya mabeki wawili na kufanikiwa kuwapita na kukimbia mbele kidogo na kupiga shuti kali lililomshinda kia wa Oljoro na kuandika goli la pili.ni moja kati ya magoli mazuri sana yaliyofungwa katika ligi ya mwaka huu.Oljoro walipata goli lao kipindi ch pili baada ya kufanya mashambulizi mengi na kufanikiwa kupata bao hilo,hadi mwisho JKT Oljoro 1 na Mbeya City 2 WELL DONE MBEYA CITY

MBEYA CITY KUWAVAA OLJORO JKT


                NA ABDUL SUDI.
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania inaendelea jumamosi hii  kwa timu ya Mbeya City,kucheza na timu ya JKT Oljoro  katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kuvutia.Timu ya JKT Oljoro ipo katika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi baada ya kushinda mechi moja na kutoa sare michezo miwili na kupoteza mitatu,wakati timu ya Mbeya City inashika nafasi ya nane ikiwa na point 8 baada ya kushinda mchezo mmoja na kutoka sare michezo mitano.
Kocha wa timu ya Mbeya City Juma Mwambusi  amesema kikosi kipo katka hali nzuri na anategemea ushindi katika mchezo wa leo,anasema hana wasiwasi na majeruhi kwani timu yake inacheza kitimu zaidi ya kumtegemea mtu mmoja mmoja “wachezaji wa Mbeya City wote wapo katika kiwango sawa,kwa vile wanacheza kitimu,hatumtegemei mchezaji mmoja mmoja ndio maana utaona hata nikifanya mabadiliko anaeingia anakua na uwezo ule ule kama wa yule aliyetoka,hivyo inakua rahisi kuunganisha na wenzake”.alisema alisema kocha  Mwambusi.
                      KILA LA HERI MBEYA CITY
       

Thursday, 3 October 2013

tatizo nini
MAN UNITED?

                               imeandikwa na Abdul(be good) Sudi,Mbeya
Kabla hajajiuzulu,aliyekua kocha wa Manchester united,sir Alex Ferguson alisema ameiacha timu ikiwa katia kiwango cha juu sana,lakini toka aje David Moyes kikosi kimebaki kile kile,lakini had sasa baada ya michezo sita imeejikuta iko katika nafasi ya 12,nafasi ya chini kuwahi kufika kwa muda mrefu sana.toka mwaka 1989.
Tatizo ni nini??hiki ndio kikosi kilichochukua ubingwa ligi kuu msimu uliopita,je tatizo n wachezaji wamechoka au tatizo liko kwa kocha David Moyes??
Ukitazama sana toka msimu uliopita timu ilionyesha kwamba inahitaji viungo,lakini hadi dakika za mwisho wakati dirisha la usajili linataka kufungwa ndio akasajiiwa Marouane  Fellaini,hivyo hajapata muda wa kukaa sana na wenzake kabla ligi hajaanza kucheza,hvyo bado anahitaji muda wa kuchanganya.
 Wachezaji wakongwe kama Ryan Gigs,Rio Ferdinand,Nemanja Vidic na hata Carrick wanashidwa kwenda na kasi ya mchezo hivyo inawapa shida sana pale wanapokutana na timu zinazojua kufanya mashambulizi ya kushtukiza “counter attack,

Kuna tatizo la majeruhi wanaotokea mara kwa mara,kama ilivyotokea kwa Rafael da Silva na kuwafanya wachezaji kama Phil Jones na Chris Smalling kupangwa pembeni hivyo kwa vile hawana mazoea ya kucheza nafasi hiyo timu inashindwa kushambulia na silaha kubwa sana kwa man ni kushambulia toka pembeni.

Na kikubwa kinachowasumbua mashabiki ni kwa nini hamchezeshi Shinji Kagawa kama kiungo wa juu,kwani alipokua Borusia Dotmund alikua akiicheza nafasi hiyo na kufunga magoli mengi mno na kutoa pasi nyingi za magoli,lakini hakuna anaeelewa kwa nini Moyes hamuamini,na hata akimpanga anamuweka nafasi ambayo si yake,pembeni kitu kinachofanya ashindwe kucheza vizuri.inashangaza kuona timu inasumbuliwa katika kiungo wakati katika benchi kuna kiungo wa kiwango cha juu.
UPANDE wa pembeni Luis Nani peke yake ndio anacheza kwa kiwango cha juu,lakini Ashley Young bado hajaonyesha kama ana sifa ya kua ni mchezaji wa timu kubwa kama ya Manchester United,na hata  Valencia sio Yule wa misimu miwili iliyopita bado hajaonyesha makali yake hivyo timu inashindwa kupata mipira ya kutokea pembeni kama ilivyokua misimu iliyopita,angalau upande wa Evra ndio anaweza kuleta  pasi kadhaa za magoli.

Ukitazama kwa makini ,kocha ana sababu nyingi sana za kulaumiwa kwani alipochukua nafasi,ilitakiwa abaki kwanza na wasaidizi wa Ferguson katika benchi la ufundi  ili wamuonyeshe njia lakini akaamua kuleta watu wapya ambao hadi sasa inaonekana wanashindwa kumshauri vizuri,ndio maana timu inasumbuka na anashindwa hata kuibadili,ikumbukwe wakati wa ferguson alikua akiweza kuubadili mchezo katika dakika 15 za mwisho,na hakuna siku hata moja Manchester iliwahi kuelemewa mwanzo hadi mwisho, ukiondoa walipocheza na Barcelona,lakini sasa hivi kila ikicheza mashabiki wake wanakua na wasiwasi,maana wanakua hawana uhakika wa ushindi.