Friday, 24 January 2014

KI MJINI MJINI
MBEYA MJINI (picha kwa hisani ya Haneef Lohaar)

Ogopa sana kuibiwa au kutapeliwa unapokua mjini, wengi wanaoibiwa au kutapeliwa ni wale wanaojiona ni wajanja sana na wa mjini sana kiasi wanajiamini kupita kiasi, wanasahau kwamba hao wezi na matapeli nao maisha yao ni ya mjini kila siku na wanaishi kwa kazi hiyo hivyo kila mara wanabadili mbinu na mitindo ya kufanyia kazi, ni sawa na mfanyakazi yeyote anaeenda kuongeza elimu chuoni,nao pia wana elimu ya mtaani wanayoongeza kila mara wanaiita “STREET WISE”……na degree yake ni ngumu kupata lakini ukiipata unakua kweli umefaulu…..