Saturday, 15 February 2014

Mbeya city sare na simba

 Mbeya City imefanikiwa kutoka sare ya goli moja kwa moja na timu kongwe na ngumu ya Simba katika mchezo mzuri uliochezwa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Friday, 14 February 2014

Mbeya city;
Ni sisi na  simba

Timu ya soka ya Mbeya City iko tayari kuikabili timu kongwe ya Simba, katika mchezo unaotegemewa kua mkali na wa kuvutia utakaochezwa jumamosi.

Wednesday, 12 February 2014

Peter mapunda
BUNDUKI YA MBEYA CITY

         Imeandikwa na Abdul Sudi, Mbeya/picha kwa hisani ya www.bayana.blogspot na Peter Mapunda.
             Mbeya City ina washambuliaji wengi,  na kila mmoja akipata nafasi anaitumia. Wengi tunamfahamu Mwegane Yeya, ana magoli matano tayari katika ligi kuu na matatu kati ya hayo aliwafunga Azam, tunamfahamu Paul Nonga, Jeremiah John na hata Richard Peter, pia tunawafahamu kina Deus Kaseke, Mohamed Kijuso na Alex Seth, wote wana uwezo mkubwa sana.