Saturday, 26 October 2013


Real yatota kwa barca

Magoli yaliyofungwa na Neymar na Alexis  yaliwafanya Barcelona kutoka na ushindi mzuri wa magoli 2-1 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Real Madrid.
          Barcelona walikua wa kwanza kupata bao katika dakika ya 19 lililofungwa na Neymar baada ya kupokea pasi toka kwa Andres Iniesta.
 Real walishambulia sana ii kupata bao la kusawazisha lakini kipa wa Barcelona alikua imara na kuzuia micho ya Khedira na Ronaldo waliokuwa na uchu wa kufunga.

      Real waliendelea kushambulia na Ronaldo alingushwa katika box la penati lakini mwamuzi hakutoa penati na baadae Benzema alipiga shuti likagonga mwamba.

                    Zikiwa zimesalia daika 12 mpira kumalizika  Barcelona walipata bao lililofungwa na Alexis Sanchez na kumaliza kabisa matumaini ya Real kusawazisha.


         Goli la kufutia machozi la Real lilipatikana katika dakika za nyongeza likifungwa na Jesse baada ya kupokea mpira toka kwa Ronaldo.
       Kiungo  Gareth Bale hakuonyesha makeke yake zaidi ya kupiga shuti kali lililotoka nje na baadae kupewa kadi ya njano kwa mchezo mbaya.   Alitolewa katika dakika ya 60 na nafasi yake ikachukuliwa na Karim Benzama aliyeongeza uhai katika timu yake.
Man utd
yashinda kwa tabu

                     Man united wamefunga magoli mawili ya haraka haraka na kunusurika na kipigo toka kwa Stoke City waliokua wakiongoza kwa magoli 2-1 hadi zikiwa zimesalia dakika 12,lakini magoli ya Rooney na Chicharito yalisaidia kupata ushindi huo.
PETER CROWCH AKISHANGILIA GOLI LA KWANZA
                  Stoke City walikua wa kwanza kupata goli katika dakika ya nne tu baada ya kipa wa  United De Gea  kuokoa mpira  uliopigwa na Peter Crowch lakini wakati Evans akijaribu kuosha ukamgonga tena Crowch na kuandika goli la kwanza.

                   De Gea alikua tena shujaa baada ya kuokoa michomo kadhaa kabla ya dakika ya  44 Robin Van Persie hajasawazisha kutokana na kichwa kilichopigwa na Wayne Rooney kuokolewa na Asmir Begovic na kumkuta  Van Persie aliyeukwamisha wavuni.
VAN PERSIE AKISHANGILIA GOLI  LA KUSAWAZISHA
                      Lakini  kabla hawajatulia, Stoke wakaongeza goli  kwa faulo iliyopigwa na Marko Arnautovic na kufanya timu hizo kwenda mapumziko Stoke ikaenda kifua mbele kwa magoli 2-1.
MARKO ARNAUTOVIC AKIFUNGA KWA FAULO GOLI LA PILI
                   Man wakashambulia sana kipindi cha pili,hasa alipoingia Adnan Januzaj kuchukua nafasi ya Nani, alibadilisha kabisa hali ya mchezo kwani waliwasumbua vilivyo Stoke na kufanikiwa kusawazisha zikiwa zimesalia dakika 12 baada ya kona ya Van Persie kumkuta  Wayne Rooney akaukwamisha wavuni.
ROONEY AKISAWAZISHA GOLI LA PILI

                  Dakika mbili baadae Chicharito aliyeinga kipindi cha pili kuchukua nafasi ya cleverly alimalizia vizuri krosi iliyopigwa na Patrice Evra na kuandika bao la tatu na la ushindi.
CHICHARITO AKIFUNGA GOLI LA TATU NA LA USHINDI
                 Mabadiliko yaliyofanywa na Man United ya kuwaingiza januzaj na Chicharito yalisaidia sana kuleta uhai kwa timu hiyo na kuepuka janga la kufungwa nyumbani.

         
 
Arsenal  yaifunga  palace

Arsenal wameweza kufanikiwa kutanua uongozi wao baada ya kuwafunga Crystal Palace kwa magoli 2-0,   moja kwa njia ya penati na Mikel Arteta  katika dakika ya 47  baada ya Sergei Gnagby kuchezewa faulo katika eneo la hatari,  na la pili likafungwa na Olivier Giroud katika  dakika ya 87 kufutia krosi safi ya Aaron Ramsey.

               Matheu Flamini na Santi Carzola walirudi kutoka majeruhi ingawa Flamini alimudu kucheza wa dakika 10 tu na kutoka baada ya kuanza kuchechemea,  nafasi yake ikachukuliwa na Gnabry.
    Arsenal walitengeneza nafasi nyingi na wakafanikiwa kupata goli  dakika mbili  baada ya mapumziko baada ya  Gnabry kuangushwa na Guedioura na Arteta kufunga kwa penati.


               Dakika ya 65 Arteta alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumvuta Maroune Charmakh aliyekua akienda kumuona golikipa, baada ya hapo hali ya mchezo ikabadilika kwani Palace walianza kushambulia na kutafuta goli la kusawazisha,lakini kipa wa Arsenal Szczesny aliokoa  mpira wa Joe Ward uliokua ukienda pembeni mwa goli na baadae akaokoa tena mpira uliopigwa na Mile Jedinaks.

          Olivier Giroud akaihakikishia Arsenal ushindi baada a kuunganisha krosi iliyopigwa na Ramsey na kumaliza ndoto za Palace za kusawazisha.
     Kwa ushindi huo Arsenal wamefikisha pointi 22 na kuzidi kujichimbia kileleni wakifuatiwa na Chelsea wenye point 17.

      

Friday, 25 October 2013

toure ataka waafrika kususia kombe la dunia


            Kiungo wa Manchestar City na Ivory Coast Yaya Toure amesema endapo UEFA  hawataichukulia hatua zinazostahili timu ya CSKA Moscow,nchi za Africa huenda zikasusia kombe la dunia la mwaka 2018 litakalofanyika Urusi. Toure aliyasema hayo mara baada ya viongozi wa soka nchini Urusi kukana kwamba hakukua na tukio la kumdhalilisha Toure au mchezaji yeyote mwenye asili ya Africa jambo ambalo limepingwa vikali na kiungo huyo.  “mimi sio kiziwi na mara kadhaa  nilimwambia mwamuzi kuwa natukanwa lakini hakuchukua uamuzi wowote kuzuia hali hiyo”alisema Toure.
WACHEZAJI WAKIMTULIZA TORE
                    Hivi karibuni shirikisho la soka ulimwenguni lilitangaza hatua za kuchukuliwa  endapo hali kama hii itatokea na ikaamuliwa mwamuzi analazimika kumaliza mchezo pindi akisikia  udhalilishaji kama huo.Raisi wa UEFA Michel Platini anasema anashangaa kwa nini mwamuzi kutoka Romania Ovidiu Hategan hakusimamisha mchezo hali hiyo ilipojitokeza na kusema uchunguzi tayari umeanza kufanyika na hatua kali zitachukuliwa kwa timu hiyo ya Urusi.
YAYA TOURE
                   Kumekua na ongezeko kubwa la udhalilishaji wa waafrika na hali inazidi kua mbaya kwani adhabu zinazotolewa zinakua ni ndogo sana kufananisha na kosa lenyewe. Klabu zinakua zinatozwa faini ndogo kiasi inakua kama vile hawajaadhibiwa.
          Katika hali ya kushangaza,mchezaji anayechezea timu hiyo ya  CSKA Moscow na raia wa Ivory Coast kama toure, Seydou Doumbia mwanzo alikaririwa akisema hakusikia milio kama ya nyani au matusi yoyote yakielekezwa kwa Toure au mwafrika yeyote,lakini baadae alikana akasema hajawahi kuongea na mwandishi yeyote juu ya jambo hilo kwa hiyo hajasema hayo maneno.Yaya Toure kwa upande wake alisema anamuheshimu sana Doumba na anajua kama aliyasema hayo maneno ni kwa sababu ya kulazimishwa na klabu yake na sio kutoka moyoni.Mchezaji mwenzake wa Manchester City Fernandinho alisema kama hali hii itaendelea na yeye atakua sambamba na waafrika kususia kombe  la dunia litakalofanyika Urusi,kwani ni jambo lisilopendeza na linakera.
SEYDOU DEMBA
             Nae kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kususia sio suluhisho kwani wanaofanya hivyo ni wachache sana na wanaopinga ni wengi ni bora zikachukuliwa hatua za haraka ili kuokoa,  kwani  kombe la dunia bila waafrika litakua si kombe la dunia tena hivyo haitakiwi wakasusa bali hatua zichukuliwe haraka kukomesha hali hiyo.
OSCAR… kiungo
 chelsea

               NI mzuri sana kwa kupiga shuti  akitumia pembeni mwa mguu (outer), anapiga chenga za haraka sana bila kufikiria kwa muda mrefu,  na anajua ni muda gani apige shuti hata akiwa mbali na goli,mara nyingi anafanikiwa kupata magoli na yanakua mazuri sana. Wengi walikua wakimfananisha na Kaka kwa jinsi anavyomudu kugawa mipira akiwa kama kiungo wa juu,  lakini ameonyesha ana uwezo hata wa kua mshambuliaji kani mara nyingi mpira unapofika katika penat box nae tayari anakua kafika.

           Oscar alizaliwa mwaka 1991  na alianza kucheza mpira katika timu ya Sao Paolo mwaka 2008, lakini mwaka 2009 aliipeleka mahakamani timu hiyo baada ya kukiuka makubaliano ya mkataba waliokuwa wameweka. Baada ya hapo alihamia timu ya Internacional alikokaa miaka mitatu hadi alipohamia Chelsea.

           Akiongelea kipajichake anasema ni kitu alichokirithi toka kwa baba yake ambae ingawa alikua na kiwango kikubwa sana lakini mazingira yalimzuia kufika mbali zaidi na pia mjombake ambae nae kama baba yake hakufika mbali ingawa alikua na kipaji.Baba yake alifariki Oscar akiwa na miaka mitatu hivyo hakuweza kumuona mwanae akiwa ni mmoja a nyota wa soka duniani.

                 “ingawa baba yangu hayupo duniani lakini nina furaha kwamba angalau mjomba yupo na anafatilia sana maendeleo yangu kwani kila nikicheza mechi lazima niikute message zake katika simu akinipongeza na kunikosoa kwa kila ninalofanya uwanjani,hua nazisubiri kwa hamu message zake na za binamu zangu,hua zinanipa faraja sana na kuiona nawakilisha familia duniani”alinukuliwa Oscar. “natamani sana kama bba yangu angekuwepo,lakini ndio hali ya dunia,huwezi kuhindana nayo,kilichopo ni kua nafanya vizuri na malengo aliyokua nayo wakati kijana mimi nayatimiza,na ninajitahidi sana kufika mbali zaidya hapa”alisema Oscar.

                         Kwa sasa Oscar amekua ni tegemeo la timu ya Chelsea kwani mara nyingi anacheza kama kiungo wa mbele,anagawa mipira na anafunga magoli muhimu kila akipata nafasi.



 

 

          

PRODUCER EPHRAIM KAMETA                           
 Wengi wamemjua Ephraim Kameta baada ya kumtoa msanii maarufu sana wa bongo flava,   Mr nice lakini Kameta hakuanza leo kufanya shughuli za muziki

Thursday, 24 October 2013

YANGA YAIFUNGA RHINO 3-0

                    Wakicheza kwa umakini,  timu ya Yanga ya Dar es salaam imefanikiwa kuwafunga Rhino Rangers ya Tabora kwa magoli 3-0,  goli moja likifungwa katika  kipindi cha kwanza na mawili kipindi cha pili katika mchezo ambao Yanga waliutawala kwa muda mwingi.
JUMA BADUL  AKIMUACHA VICTOR HANGAYA WA RHINO

    Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa aliwasumbua sana walinzi wa pembeni wa Rhino kwani hawakua na njia nzuri ya kumzuia na kumfanya apige pasi na krosi nyingi kuelekea langoni mwa Rhino.  Na Simon Msuva alianza mchezo huo vizuri na kwa umakini mkubwa lakini kadri muda ulivyozidi kwenda alipoteza umakini na kufanya maamuzi mengi ambayo hayakua na uhakika,na akawa anajiangusha ili  apate faulo matokeo yake akapewa kadi ya njano. Alikuja kutolewa katika dakika ya 59.
            Yanga walibadili kikosi chao tofauti na kilichozoeleka na ambacho kilicheza na Simba katika sare ya 3-3,  walimuweka Juma Abdul kama beki wa kulia badala ya Mbuyu Twite aliyecheza beki wa kati,  na Zahir Rajab katika kiungo wa chini nafasi ya Atumani Iddi na mbele akaingia Simon Msuva  ambae alicheza pembeni na  katikati akasimama Hamisi Kiiza na Mrisho Ngasa,hivyo Athumani Iddi,Didier Kavumbagu na Nadir haroub hawakupangwa kabisa,na golini alikuwepo Deogratius Munishi badala ya Ally Mustafa.
HAMISI KIIZA AKISHANGILIA GOLI
             Goli la kwanza la Yanga lilipatikana baada ya Simon Msuva kupokea mpira toka kwa Zahir na akakimbia pembeni akimuacha kirahisi beki wa kushoto wa Rhino Hussein Abdallah na kupiga krosi iliyompita Ladislaus Mbogo na kumkuta Kiiza aliyeupeleka wavuni,ilikua ni dakika ya 12. Waliendelea kutawala na kuwapoteza kabisa viungo wa Rhino Stanslaus Mwakitosi,Imani Ndeli na Nurdin Bakari ambao muda mwingi walikua wakiutafuta mpira bila mafanikio.
               Yanga walifanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 72 lililofungwa na kiungo wao Frank Domayo aliyemalizia kazi nzuri ya Mrisho Ngasa aliyempita kwa umaridadi beki wa kushoto WA Rhino na kutoa pasi nzuri kwa Domayo aliyemalizia kirahisi.Rhino hawku na mipango ya kutafuta goli kwani hata golikipa wa Yanga Meogratius Munishi  hakuokoa hata hatari moja,muda wote wa mchezo alikua kama mtazamaji.
MBUYU TWITE AKIMDHIBITI IMANI NDELI

                   Goli la tatu lilifungwa tena na Hamisi Kiiza na kumfanya afkishe magoli saba katika ligi hii,lilipatikana baada ya mpira ulioppigwa na Ngasa kumshinda Nurdin Bakari aliyeteleza na kuanguka na mpira kumfikia Kiiza aliyeupeleka pembeni mwa goli la Rhino na kuandika goli la tatu.Kwa ujumla Yanga walicheza vizuri sana katika mchezo huo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga tofauti na Rhino ambao walikua kama hawajajitayarisha kwa ajili ya mchezo huo.
HAMISI KIIZA,DOMAYO,NIZAR NA NGASA 

            VIKOSI;
  YANGA-Deogratius Munishi,Juma Abdul,David Luhende,Mbuyu Twite,Kelvin Yondani,Zahir Rajab,Simon Msuva,Frank Domayo,Hamisi Kiiza,Mrisho Ngasa,na  Haruna Niyonzima.
   RHINO- Mahmoud Othman,Ally Mwanyiro,Hussein Abdallah,Julius Masonga,Ladislaus Mbogo,Stanslaus  Mwakitosi,Shija Mongo,Imani Ndeli,Victor Hangaya,Saad Kipanga na Nurdin Bakari.


                     

Tuesday, 22 October 2013



JUMA MWAMBUSI;
MTAALAM WA MBEYA CITY

                                        KOCHA JUMA MWAMBUSI 
   
     Kila mpenda soka Tanzania sasa hivi lazima anaijua timu ya Mbeya City,na wanaijua si kwa vile inashiriki tu ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,lakini kutokana na kiwango cha hali ya juu kinachoonyeshwa na timu hiyo.Wanakaba kwa pamoja,wanashambulia pamoja na wanashirikiana kwa kila hali wakiwa uwanjani,hilo limezisumbua sana timu pinzani  kila wanapokutana nazo.
            Yote hayo yanafanikiwa kutokana na ubora wa kocha anaefundisha timu hiyo,Juma Mwambusi,kwani anakazania sana soka la kushirikiana. “sipendi timu ninayofundisha iwe na nyota mmoja au wawili na kuwameza wachezaji wengine,huwa nawatayarisha wachezaji wangu wote wawe nyota,wategemeane na washirikiane  kiasi hata mmoja  asipocheza aingie ambae ana kiwango kile kile kama cha  wengine”alisema  Juma Mwambusi alipoongea na mbeyamaskan’ “nina wachezaji wengine zaidi ya kumi na nane wana kiwango sawa sawa na hawa wanaocheza sasa hivi,hivyo sitegemei timu yangu iwe kama nguvu ya soda,tumejipanga vizuri”.

              Akaendelea “Unajua siri ya kua mchezaji mkubwa  na mzuri ni nidhamu,kweli wapo wachezaji wengi duniani wenye nidhamu mbovu na lakini ni mahiri na maarufu sana katika soka,nidhamu ninayoisema mimi ni ile ya kupenda na kuheshimu kile unachokifanya,kufika kwa wakati mazoezini, kufanya mazoezi kwa bidii pale unaposimamiwa na hata ukiwa peke yako,na kujifunza kwa bidii kile kinachokushinda ukiwa uwanjani,na hata unachokiweza kukifanyia mazoezi zaidi ili kisije kukutoka,hiyo ndio nidhamu ninayoisema,”aliongeza.
                                              KOCHA MWAMBUSI

        Juma ambae ni mpole na mcheshi sana akiwa katika maisha ya kawaida,lakini ni mkali na makini sana anapokua katika kazi yake ya ukocha aliendelea“Ili timu iwe na mshikamano lazima kocha uwe na msimamo,usipende kua mkali sana kila mara ili wakuogope,hapo watakua na nidhamu ya uoga na ni rahisi sana kukutania na kutokua makini pindi unapowapa mgongo,na haitakiwi uwe mpole kwani watakua huru sana na mwisho wa siku wote mtaonana mko sawa,kutakua hakuna kiongozi tena”aliendelea kunambia.
     “Kwa hiyo siri yangu kubwa sana ni nidhamu,nataka mchezaji ninaemfundisha ajue anataka nini,ajue anatakiwa afanye nini na pia nataka ajali anachokifanya,hapo tutakua sawasawa,na nina hakika mchezaji mwenye nidhamu lazima atafika mbali sana tofauti na wasio na nidhamu.”
    Juma Zakaria Mwambusi alizaliwa mkoani Mbeya na kupata elimu yake hapo hapo Mbeya,Alipomaliza High School akaanza taratibu kujiingiza katika kozi za awali za ukocha zilizokua zikitolewa na FAT hadi TFF na kupata vyeti kadhaa,haikutosha akaamua kwenda Ulaya ili kuongeza ujuzi na mwaka 2001 akapata DIPLOMA nchini Hungary,na baadae akapata tena DIPLOMA ya kua instructor iliyotolewa na shirikisho la osoka ulimwenguni,FIFA hapa hapa Dar,na mwaka jana amefanya kozi na kufanikiwa kupata licence B ya CAF.hivyo si kocha wa kubahatisha ni kocha aliesomea.
                 Timu alizowahi kufundisha kwanza kabisa ni TUKUYU STARS mwaka 2002 na kufanikiwa hadi kufika katka timu nane bora  na yeye akachaguliwa kuwa ni kocha bora,vilevile TUKUYU STARS ikachaguliwa kua ni timu yenye nidhamu.
Mwaka 2003 akaifundisha timu ya PALSON ya Arusha nayo pia ikaingia hadi nane bora.Na mwaka 2005 alikua ndie kocha wa timu ya mkoa wa Mbeya ya Mapinduzi Stars na wakafanikiwa kuchukua kombe la taifa,mwaka 2007/2008 alikua ni kocha wa timu ya PRISON ya Mbeya,wakashika nafasi ya pili katika ligi kuu na pia akachaguliwa kua ni kocha bora,na mwaka 2001 akawa tena kocha wa timu ya mkoa wa Mbeya Mapinduzi Stars na wakafanikiwa kutwaa ubingwa wa taifa na pia akachaguliwaa kua ni kocha bora wa mashindano.
                                              JUMA MWAMBUSI
           
    Sasa hivi ni kocha wa Mbeya City,timu ambayo tayari imeonyesha sura tofauti ya mchezo wa soka hapa Tanzania,kwani walipoanza mchezo wa kwanza walitoka sare na Kagera,wakaja kuifunga Ruvu Shooting kisha wakatoka sare na Yanga ,wakatoka tena sare na Mtibwa,Simba,Coastal Union,na baadae wakazifunga Oljoro,Rhino,Mgambo na Ruvu JKT.na kila siku timu inazidi kuonyesha ukomavu na kuzoea mikiki mikiki ya ligi kuu.
                                    MWAMBUSI AKIWA NA MSAIDIZI WAKE.


         Alipoulizwa kama wana nia ya kuchukua ubingwa wa Tanzania alisema “tunataka  twende hatua kwa hatua,tunajitayarisha tu na mchezo unaokuja  mbele yetu,hivyo tukifanya vizuri katika huo mchezo tunaanza kujitayarisha na mchezo unaofuata,hatutaki kujichanganya na mambo mengi wakati kuna kazi kubwa ya kufanya hivyo tukifanikiwa kuzifunga timu tunazokutana nazo basi na ubingwa utakuja,lakini sio kazi ya kusema tu kwa mdomo kwamba nataka kua bingwa,inabidi ifanyike sana kazi,sasa hivi nimeanza kupata wasiwasi na waamuzi wanaochezesha hii ligi,sijui kama ni kwa makusudi au kutokujua lakini maamuzi yao mengi yanakua ni ya mashaka.mfano tulifunga goli zuri sana siku tumecheza na Mgambo lakini kwa maajabu mwamuzi akalikataa,hadi leo sijui sababu ya kulikataa hilo goli,hivyo kuna kazi kubwa sana mbele zaidi ya huku tulikotoka,ila nawashukuru sana wapenzi wa soka jijini Mbeya,wanatupa sapoti kubwa sana kiasi kila siku tunajiona tuna deni la kuwalipa,na kuwalipa ni sisi kujitahidi kucheza vizuri na kushinda michezo yetu,nawashukuru sana wachezaji wangu,kwani wamekua wasikivu mno na wamefanikiwa kucheza vizuri hata katika mechi zenye presha kubwa,kwa hilo wanastahili sifa”alimalizia Juma Mwambusi.

Monday, 21 October 2013






Simba
Ilivyo chomoa
kwa
yanga
      NA ABDUL SUDI.
KIKOSI CHA SIMBA

                   Wakati wa mapumziko,kila shabiki wa mpira Tanzania,iwe anatazama akiwa uwanjani au katika televisheni,au awe anasikiliza katika radio aliamini kabisa Yanga wameshashinda mchezo huo,kilichokua kikisubiriwa ni idadi ya magoli yatakayoongezeka kipindi cha pili.kwani pamoja na kuongoza kwa magoli matatu walikuwa wameutawala mchezo katika idara zote,katikati Athumani Iddi,Frank Domayo na Haruna Niyonzima walikua wamepashika vilivyo.Mrisho Ngasa na Didier Kavumbagu walikua wanasumbua sana,na Hamisi Kiiza alikua akirudi kuwasaidia viungo na kuipeleka mipira mbele na kwa kasi waliyoku nayo Yanga,mchezo ulionekana tayari umekwisha.
KIKOSI CHA YANGA
                                                                                  
             Lakini sio kwa Kibaden na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo,wao walikua na imani kua mambo yanaweza kubadilika,walitulia wakatazama nini tatizo,wakaona wametawaliwa katikati wakaamua kufanya mabadiliko yaliokua na manufaa makubwa katika mchezo huo,wakamtoa Chanongo ambae hakucheza katika kile kiwango alichozoeleka,wakamtoa na Humud ambae kwa vile alichezeshwa nafasi ambayo hakuizoea ya kiungo wa mbele, ilikua inamuwia ngumu sana kugawa mipira,alikua anakaba vizuri lakini anapotoa pasi alikua mara nyingi anawapasia maadui hivyo kufanya Jonas Mkude aliyecheza kiungo wa chini awe na kazi ngumu sana ya kuitafuta mipira iliyoharibika.
     Wakawaingiza watoto Wiliam Lucian,na Said Ndemla ambao kwa kiasi kikubwa ndio waliobadili sura ya mchezo.walisaidiana kukaba na kugawa mipira vizuri sana na kumfanya Mkude awe na sehemu kubwa sana ya kucheza katikati,na kutokana na kuchoka kwa Athumani Iddi Simba walitawala mno kiungo katika kipindi cha pili.na wakatengenza nafasi nyingi za kufunga na wakafanikiwa kuzitumia tatu kati ya hizo.
OWINO(KUSHOTO JEZI NYEKUNDU)AKIFUNGA GOLI LA PILI
Yanga walianza mchezo huo kwa nguvu sana kwa kupiga pasi nyingi na kuwachanganya Simba.na  kufanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika ya 14 baada ya kazi nzuri sana iliyofanywa na Didier Kavumbagu kuwazidi nguvu na ujanja mabeki wawili wa Simba ambao walimfuata kwa pamoja na kumuacha Kiiza pembeni,hivyo Kavumbagu alivyogombea nao mpira alifanikiwa kuusogeza hadi kwa Kiiza ambae alipiga krosi na kipa wa Simba alitaka kutoka akasita na ndipo mpira ukamkuta Mrisho Ngasa aliyepiga mini volley na mpira kupita pembeni juu ya lango la Simba na kuandika bao la kwanza.

       Hawakuachia hapo kwani waliendelea kushambulia na kufanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Hamisi Kiiza baada ya mabeki wa Simba kushindwa kuuzuia mpira uliorushwa na Mbuyu Twite na kumkuta Kiiza aliyeusukumiza wavuni.Simba wakapoteana na Yanga wakazidi kucheza kwa uhakika,Chanongo akawa anashindwa kumsaidia Haruna Shamte ambae muda mwingi alijikuta anaingia katikati kwenda kuwasaidia mabeki na viungo hivyo pembeni Ngasa akawa huru sana,Athumani Iddi akawa anapiga pasi pembe zote na Niyonzima akasogea sana katikati na kuwafanya viungo wa Simba kushindwa kuhimili nguvu kubwa ya Yanga.
MOMBEKI AKIWAHI KUANZISHA MPIRA BAADA YA GOLI LA PILI LILILOFUNGWA NA OWINO
                Goli la tatu la Yanga lilipatikana kutokana na uzembe uliofanywa na Ramadhan Singano  baada ya kupata pasi kutoka kwa Cholo akataka kupiga chenga lakini hakuweza hivyo akataka kuurudisha kwa Cholo kwa kisigino na Yanga wakaunasa na wakapiga mpira mrefu uliomkuta Kavumbagu aliyemzidi mbio Cholo na kutoa pasi kwa Kiiza aliyeukwamisha wavuni na kuandika goli la tatu.
               Wachezaji wa Yanga wakaona wamemaliza mchezo wakawa wanacheza kwa mbwembwe  na hasa Mrisho Ngasa na Nadir Haroub,wakawa  wanaucezea mpira wanavyotaka,hawakujua kua wanawapa Simba nafuu kwani tayari walikua wamepoteana.
Hadi mapumziko Yanga wakawa wanaongoza kwa magoli matatu kwa bila.
                Kipindi cha pili Simba walifanya mabadiliko baada ya kuwatoa Humud na Chanongo n nafasi zao kuchukuliwa na Said Ndemla na Wiliam Lucien ambao wakaubadilisha mchezo kwa kila hali.Wakamsaidia Mkude kukaba katikati na kuvuruga mipango ya Yanga,na kwa vile Athumani Iddi alikua tayari kachoka akawa anacheza nyuma sana hivyo kuwafanya viungo wa Simba kummeza Domayo,na Niyonzima akawa hapati tena mipira toka katikati.wakafanikiwa kupata bao la kwanza kupitia kwa Betram Mombeki aliyepata pasi nzuri toka kwa Hamis Tambwe aliyekimbia na mpira hadi pembeni mwa lango la Yanga  na kupiga pasi iliyomkuta Mombeki na akaupiga kiufundi na kuandika bao la kwanza.
KELVIN YONDANI AKIWA HAAMINI
                   Simba wakazidi kuchangamka na Yanga wakapoteana,kwa vile Niyonzima alikua akiingia sana katikati,Nassor  Cholo akawa huru sana upande wa kulia na kumfanya muda mwingi kucheza kama mshambuliaji,na alisababisha matatizo mengi sana kwa mabeki wa Yanga, kwani magoli yote yalitokea upande wa kulia.
     Goli la pili lilitokana na kona upande huo huo wa kulia na Ramadhani Singano alipopiga hiyo kona ilimkuta Josef Owino aliyepiga kichwa na kuandika goli la pili.Yanga wakaamua kumtoa Kiiza na nafasi yake kuchukuliwa na Simon Msuva,mabadiliko yaliyowamaliza kabisa nguvu Yanga kwani hawakuwa tena na mipango ya kushambulia.Msuva na Ngasa wote wakawa wanacheza upande wa kulia na Niyonzima akawa kaingia sana katikati hivyo pembeni upande mmoja  kwa Yanga hakukua tena na mtu,Simba wakawa wamekamata kabisa katikati.
    Ngasa alipata nafasi ya kumaliza mchezo baada ya kuwatoka mabeki wawili wa Simba lakini uhodari wa kipa wa Simba Abel Dhaira ulimkosesha goli kwani aliokoa ikawa kona ambayo haikuzaa matunda.
GILBERT KAZE

                   Simba walipata bao lao la tatu kupitia kwa beki  wake wa kati Gilbert  Kaze baada ya faulo iliyotokea upande ule ule wa kulia ikapigwa na Nassor Cholo na kumkuta Kaze akiwa hana mtu wa kumkaba kwani mabeki wawili wa Yanga walikua wamemkaba Mombeki na hivyo Kaze akapiga kichwa na kuandika bao la tatu.

WACHEZAJI WA YANGA WAKILAUMIANA BAADA YA KUINGIA GOLI LA TATU
                              Simba wakapata sare ambayo wala hawakuitarajia.kwa kiasi kikubwa yanga walitakiwa kushinda hii mechi lakini hawakua makini katika kuulinda ushindi wao na kudhania mechi tayari imekwisha.