Saturday, 1 March 2014

yanga
yawaduwaza al alhly

      Klabu bingwa ya Tanzania Yanga, leo imevunja mwiko baada ya kuwafunga Al Ahly yaa Misri goli moja kwa bila katika mchezo wa klabu bingwa Afrika. Toka waanze kukutana mwaka 1982, hii ni mara ya kwanza kwa Yanga kushinda.

Friday, 28 February 2014

YANGA VITANI NA AL AHLY

Yanga ya Tanzania, jumamosi inakutana na mabingwa wa Misri Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa klabu bingwa Africa, Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Monday, 24 February 2014

PETER MICHAEL
wa tz prisons

    Katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, timu ya Tz Prisons haikua inaenda vizuri, ilikua inasua sua mno, baadae wakaamua kubadili benchi la ufundi kwa kumuondoa kocha Jumanne Chale na kumleta kocha mzoefu David Mwamaja. Hali hiyo kwa kiasi Fulani imeleta mabadiliko kwani katika michezo mitano ya mzunguuko wa pili, imetoka sare miwili na kushinda mitatu.

Sunday, 23 February 2014

Tz prisons wako vizuri….

Timu ya Tz Prisons imetoka sare ya kufungana magoli mawili kwa mawili na timu ngumu ya Azam fc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Azam compex Chamazi.