Miaka kadhaa iliyopita mkoa wa Mbeya
ulikua ukisifika kwa kutoa wachezaji wazuri na wengi waliokuwa wakienda
kuchezea timu mbali mbali kubwa za hapa nchini,Kuanzia kina Rajab Muhoza na
Mtawa Kaparata waliokwenda kuchezea Maji Maji ya Songea kwa vipindi
tofauti,kina Justin Mtekere,Salum Kabunda,Sekilojo Chambua,Suleiman Mathew,Godwin
Aswile,Mbwana Makata na Steven Mussa waliokwenda Yanga na kua ni wachezaji
maarufu sana nchini,kina Aston Pardon,Michael Kidilu,Maumba Mikidadi
waliokwenda Simba na wengine wengi waliokwenda timu tofauti kutoka mkoani
Mbeya.Na hilo lilitokana na kuwa kulikua
na uongozi imara wa chama cha soka
mkoani Mbeya uliokua ukiongozwa na
mwenyekiti marehemu mzee Aban Nusura uliokua umesimama imara kuhakikishaTukuyu
Strars inapanda daraja toka daraja la tatu hadi kua bingwa wa Tanzania na timu
tishio sana hapa Tanzania, ilikua si ajabu timu kubwa kutoka Malawi au Zambia
kuja Mbeya kucheza michezo ya kirafiki,timu kama Nkana Red Devils na Mufulira
wonderers zilikua zikija mara kwa mara na kuna mwaka hata timu kutoka Denmark
ilikuja na kuonyesha burudani safi sana kwa wakazi wa Mbeya.Hizo zote zilikua
ni changamoto kwa timu za Mbeya za wakati ule ili kuzipa mazoezi na uzoefuwa
kucheza michezo mikubwa.Na mafanikio yalionekana kwani timu kama Tukuyu Stars
ikafanikiwa kupanda daraja hadi kuchukuaa ubingwa.
Mashabiki wa mkoa wa Mbeya wana
nafasi kubwa sana kwa mafanikio ya timu hiyo ya Tukuyu Stars na hata
Mecco,kwani wakazi wa Mbeya wana sifa ya kupenda timu zao,na mar azote hua
wanazipa sapoti ya asilimia kubwa sana,ni nadra sana kukuta mtu wa Mbeya
aliyezaliwa Mbeya akiishanglia timu toka nje,mara nyingi wanaoshangilia timu
pinzani wanakua ni watu wa kuja si wazawa wa Mbeya.Ndio maana hata timu ya
Prison mwanzo ilikua na mashabiki wengi sana
lakini hali ikabadilika baada ya uongozi kuamua kusajili wachezaji wengi
toka katika magereza morogoro na kuacha vijana wengi toka mkoani Mbeya hivyo
wakazi wa Mbeya wakaona kama wamesalitiwa na kuamua kuacha kuisapoti timu
hiyo.Ingawa sasa hivi hali imebadilika baada ya kuamua tena kuisapoti timu hiyo
na ni baada ya kusajili tena wachezaji wengi toka mkoani mbeya.
Sasa hivi imekuja timu kipenzi cha wakazi wa Mbeya,timu ya MBEYA
CITY,timu ambayo imepanda daraja msimu huu na kua inacheza katika ligi kuu ya Tanzania.Kutokana na usajili wake ulivyokua
mzuri na jinsi walivyofanikiwa kupanda daraja kabla hata ligi
haijaisha,kumewafanya wakazi wa mbeya kua na imani kubwa sana na timu hiyo.na
hata katika mech zao za mwanzo imeonyesha ina dhamira ya kushindana si kuwa
msindikizaji.nilipoongea na baadhi ya wakazi wa Mbeya kusu timu hiyo,hawakusita
kueleza furaha na mapenzi wwaliokua nayo kwa timu hiyo,na wengi walieleza
matumaini ya kuja kua ni moja kat ya timu bora sana hapa Tanzania.Nilipotembelea
eneo maarufu kwa biashara eneo la Mwanjelwa nilikutana na mfanya biashara wa
nguo ambae alikua akiuza jezi za timu ya Mbeya City,mfanyabiasahara huyo aitwae
FESTO DOMNGO alinambia “hii ni timu halisi
ya mkoa wa Mbeya kwani hata wachezaji wengi waliosajiliwa ni wa hapa hapa
Mbeya,hivyo tunawajua toka wanaanza
kucheza mpira na tulikua tunawafatilia na kuwaona ni wazuri sasa wamesajiliwa
na timu ya hapa mkoani sina budi kuishangilia na kuona ni yetu kabisa wakazi wa
Mbeya,ninaipa sapoti kwa asilimia mia”alinambia huku akiibusu jezi yake
aliyovaa ya Mbeya City.
FESTO DOMINGO
JOSEPHAT MWAKALEKANE
Shabik mwingine aliyejulikana kwa jina la AMBWENE MWAKALOBE
yeye alisisitiza tu kua “ninaiamini sana timu ya MBEYA CITY,huyu ndio mkombozi wa soka la Mbeya
kwani wanajituma sana na wachezaji wana nidhamu hata ukiwatazama mazoezini
unaona wana dhamira ya kufika mbali,ninawaommbea kwa mungu wafanikiwe na kuutoa
kimasomaso mkoa wetu wa Mbeya”
AMBWENE MWAKALOBE
Hata niliotembelea eneo la kabwe katika sehemu
ambayo ina maduka ya kuuza viatu,hapo nilikutana na mashabiki wengine waaliokua
wamevaa jezi za MBEYA CITY,na niliongea nao na wakawa na haya ya kusema.
“wakazi wa Mbeya tunapenda sana soka,na kila mara mkoa unakua na wachezaji
wengi sana maana hata ukitazama kuna mashindano mengi sana yasio rasmi
yanayoendeshwa hapa mkoani,na ukitazama vwango vinavyoonyeshwa na hao vijana ni
vya hali ya juu sana ndio maana hatujashangaa kuona timu ya MBEYA CITY ikichukua
wachezaji wengi toka hapa hapa mkoani,na mimi ni mkazi wa Mbeya lazima niipende
timu yangu,naona rah asana kuwatazama madogo wa mtaani wakiichezea timu ya
nyumbani”alinieleza FRANK MWAMBENE mfanyabiashara wa viatu hapo sokoni kabwe.
FRANK MWAMBENE





