Saturday, 19 October 2013

 MAN UTD YABANWA TENA

Kwa mara nyingine timu ya Manchester united imeshindwa kupata ushindi nyumbani baada ya kulazimishwa sare na timu ya Southampton kwa kufungana goli 1-1.
    Suthampton walipata bao lao ikiwa imesalia dakika moja mpira kumalizika kwa goli lililofungwa na beki Dejan Lovren na kuzima ndoto za Man za kuondoka na ushindi.
             Man walikua wa kwanza kupata goli lililofugwa na RobinVan Persie baaada ya kazi nzuri iliyofanywa na kinda Adnan Januzaj  na kumpasia Rooney aliyepiga na kipa wa Southamton akashindwa kuuhiili na kumrudia Van Persie aliyeukwamisha wavuni.

   Van Persie tena nusura aipatie Man goli la pili lakini mpira aliopiga kichwa ukagonga nguzo.


     Baada ya mchezo kocha wa timu ya Southmpton Mauricio Pochettino alisema ameridhika na sare hiyo ingawa kulikua nafasi ya kuweza kushinda lakini kwa kupata sare ni jambo kubwa sana ukichukulia unacheza katika uwanja kama wa Old Traford. Nae kocha wa man David Moyes  alisema timu yake ilifanya kosa kuridhika na goli moja na hilo ndio tatizo kwani w
alipata nafasi wakashindwa kuzitumia hivyo wamestahili kupata hiyo sare.
 USIOMBE KUKUTANA NA
MBEYA CITY,ni BALAA….
     NA ABDUL SUDI,MBEYA

                                                                         wahamasishaji wa mbeya city
MBEYA CITY leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga timu ya JKT  stars kwa goli 1-0 katika lig kuu ya Vodacom Tanzania bara,huu ni mchezo wa nne mfululizo kwa timu hiyo kushinda baada ya kuzifunga timu za Oljoro JKT 2-1,Rhino Rangers 3-1,kisha kuwafunga Mgambo JKT 1-0 na sasa kuwafunga JKT Stars 1-0.
         Goli la ushindi kwa Mbeya City lililofungwa na mshambuliaji wake hatari Jeremiah John katika dakika ya 30 ya mchezo baada ya kona iliyookolewa na walinzi wa JKT na mpira kumkuta mfungaji aliyepiga shuti kali lililotinga wavuni.
           Mbeya City itajilaumu kwa kukosa magoli mengi ya wazi hasa kipindi cha pili kwani waliutawala mno mchezo na kushinda golini mwa JKT lakini uhodar wa kipa na kutokua makini kwa washambuliaji wake kuliifanya timu hiyo kumaliza mchezo na goli hilo hilo moja,
            Kocha wa timu hiyo Juma Mwambusi  kama kawaida aliwashukuru sana mashabiki wa timu hiyo kwa kuwapa sapoti kubwa na pia aliwashukuru wachezaji wake kwa kujituma na kuweza kufanikisha ushindi huo.
           Kwa ushindi huo timu ya Mbeya City imefikisha pointi  20 sawa na Azam na kuongoza ligi hiyo kwa muda.

                                                        KIVYETU VYETU
 Na katika mchezo mwingine wa ligi hiyo,timu ya Mtibwa imeifunga  Mgambo JKT kwa magoli 4-1 mchezo uliochezwa  katika uwanja wa manungu.magoli ya Mtibwa yalifungwa na Shaaban Nditi aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Awadh  Juma  ,na goli la pili lilifungwa na mchezaji chipukizi  Juma Luzio baada ya kupata pasi ya shaaban nditi,na goli la tatu lilifungwa tena na  Juma Luzio  baada ya kupata mpira katikati ya uwanja na kuwapita mabeki wa mgambo  kisha akakimbia  na kupiga shuti kali la mguu wa kushoto lililomshinda kipa wa Mgambo Kaviche  na kuingia.Goli la nne lilifungwa na Shaaban  Mkopi.Mgambo walikuja kupata goli la kufutia machozi kupitia kwa   Nguya dakika ya 83 kwa njia ya penati baada ya mshambuliaji wake kuangushwa katika eneo la hatari.      
Nayo timu ya Kagera  Sugar imefanikiwa kuifunga timu ya Coastal Union ya Tanga kwa goli moja lililofungwa na Salum Kanon kanon  dakika  ya 60 kwa njia ya  penati.         
Azam wameifunga JKT Oljoro ya Arusha  goli moja liliofungwa na kiungo wake Mcha Khamis katika dakika ya 67.


   Nayo Ashanti imelazimisha sare ya magoli 2-2 na timu ya Ruvu Shooting katika mchezo uliochezwa uwanja wa AZAM,Ruvu ilikua ya kwanza kupata magoli yake yote mawili moja kila kipindi yaliyofungwa na lakini Ashanti walikuja kuzinduka dakika 20 za mwsho na kufanikiwa kusawaziha magoli yote mawili.

Friday, 18 October 2013

Mbeya city uso kwa uso na jkt ruvu
                                                                                      NA ABDUL SUDI


                                                                             SHABIKI WA MBEYA CITY
Timu ya Mbeya city iliyo katika form kali,jumamosi inapambana naJKT ruvu katika mfululizo wa michezo ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania.Katika michezo yake iliyopita Ruvu stars ilifungwa magoli 3-0 na Azam na kabla ya hapo walikua wamefungwa naSimba2-0,kisha na Mtibwa 2-1 hivyo watakua wanatafuta kwa nguvu sana ushindi ili uweza kujiweka katika nafasi nzuri.
                   Mbeya city wana kumbukumbu nzuri ya ushindi mfululizo katika michezo yake kwani katika michezo mitatu iliyocheza ugenini  imefanikiwa kujipatiapoint zote tisa kwakuwafunga JKT Oljoro 2-1mjini Arusha,kisha wakawafunga Rhino yaTabora 3-1na mwisho wamewafunga  Mgambo JKT kwagoli 1-0.Hivyo wako ktika kiwango kizuri na ukichukulia wanacheza katika uwanaja wao wa nyumbani ulio na sifa ya kujaza mashabiki wake wanaoisapoti timu hiyo kwa kuishangilia mwanzo hadi mwisho.
                Akielezea mchezo huo,kocha wa timu ya Mbeaya City Juma Mwambusi amesema wanauchukulia kwa tahadhari kubwa sana mchezo huo kwani kwa vile wameshashinda mechi  tatu mfululizo wanajua wapinzani wao watakua wamejipanga vilivyo kujilinda  na kufanya mashambulizi ya kushtukiza,hivyo amewaambia vijana wake watashambulia mwanzo hadi mwisho ili wawezekuondoka na point tatu muhimu katika mchezo huo,aliongeza hadi sasa timu iko vizuri na hakuna majeruhi wa kutisha katika timu hiyo,hivyo wapenzi na mashabiki wa soka jijini hapa wategemee mchezo mzuri na Insha allah timu itashinda.

         Michezo mingine inayotarajiwa kuchezwa mwisho wa wiki hii ni  Kagera sugar watawakaribisha Coastal Union,JKT Oljoro watacheza  Azam,wakati Mtibwa sugar watakua wenyeji wa Mgambo shooting,na Ashanti watacheza na Ruvu Shooting.jumapili ni Simbana Yanga.

Monday, 14 October 2013

OZIL
 Atabiriwa kuwapa
arsenal ubingwa

Kiungo wa timu ya Arsenal Saint Carzola anaamini ujio wa mtaalam Mersut Ozil katika klabu hiyo umewapa hamasa wachezai wengine kupigania ubingwa na kumaliza ukame wa makombe.
          Kocha wa Arsenal,Arsene Wenger alivunja rekodi za gharama za usajili wa timu hiyo baada ya kumchukua Ozil kutoka Real Madrid dakika za mwisho za dirisha dogo la usajili ka gharama ya paundi milioni 42.
           Carzola anasema bado anashangaa kwa nini Real Madrid walimuachia mchezaji mwenye kiwango bora kama cha Ozil na alifurahi sana kumuona akijiunga na Arsenal.

      “nilishangaa sana kusikia Madrid  wanamuacha na nilifurahia mno kuona mchezaji mwenye kiwango kama chake anakuja kucheza na sisi,na alipokuja hakua na makeke yoyote,alikuja na kuanza kufaya kazi mara moja,ni mchezaji ambae unajifunza mengi sana toka kwake,na ni mtaalamu sana”alisema Carzola.
           Akimuongelea Ozil mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Robert Pires amesema “Ozil ameleta kitu ambacho kilikua kinahitajika muda mrefu sana,Arsenal wamezoeleka kwa kukaa sana na mipira lakini hawako makini kwa kutoa pasi za mwisho lakini sasa amekuja Ozil anaifanya hiyo kazi na kuwarahisishia wengine kufunga kirahsi,hadi sasa tayari kafunga na kutoa pasi tatu za magoli,ni kiwango kizuri sana  

          Kocha Arsene Wenger yeye anasema  kuja kwa Ozil kumeamsha ari kwa wachezaji wengine wa Arsenal,ni usajili sahihi ambao malio yake yankuja pale pale bil kusubiri muda.
    Ozil alicheza michezo 105 akiwa Werder Bremen na kufunga magoli 16 n kutoa pasi za mwisho 55,alipokwenda Real Madrid alifunga magoli 27 akatoa pasi 81 katika michezo 159 na kumfanya awe ni kiungo mshambuliaji bora  katika ligi zote za ulaya kwa msimu uliopita.na wengi wanaamini alikua ni kiungo mshambuliaji bora duniani msimu uliopita.


Sunday, 13 October 2013

mbeya city......MADE IN MBEYA……..

                            na abdul sudi.

                Timu ya soka ya Mbeta City imefanikiwa kuendeleza wimbi la ushindi ugenini baada ya kuifunga timu ya Mgambo shooting kwa goli moja kwa bila,kabla ya mchezo huo Mbeya City iliwafunga  Oljoro JKT ya Arusha 2-1,ikawafunga tena Rhino ya tabora kwa magoli 3-1 na leo tena imewafunga Mgambo shooting goli moja bila.katika mchezo wa leo goli la Mbeya City lilipatikana katika kipindi cha kwanza likifungwa na mshambuliaji wake hatari Jeremiah Juma.kpindi cha pili Mgambo walijitahidi kulishambulia lango la Mbey a City ili upta bao la kusawazisha lakini uhodari wa ngome ya City uliwanyima nafasi ya kumfikia kipa wao.Akiongea baada ya mchezo kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi alisema anashukuru vijana wake wamepigana na kufanikiwa kupata point zote tatu na sasa hvi anatazama mchezo ujao ambapo watacheza nyummbani na timu ya JKT Ruvu.aliwashukuru mashabiki wa soka wa moa wa Mbeya waliosafiri kuifata timu yao na kuwaahidi vijana wake watafanya kila wawezalo ili kuzidi kufanikiwa.

Mbeya City inatarajia kucheza na Ruvu JKT tarehe 19  mwezi huu jijini Mbeya na tarehe 26 mwezi huu watakua na kazi nzito ya kukutana na ndugu zao wa TZ Prisons katika mechi inayotaraiwa kuvutia maelfu ya wakaziwa jiji la Mbeya.