Mnara wa Uhuru ndio kama kitambulisho cha mkoa wa Mbeya,upo
katika eneo la mjini karibu kabisa na kikosi cha Zimamoto,ofisi ya mkuu wa
mkoa,ofisi za mkuu wa wilaya(bomani)na si mbali sana na ofisi za halmashauri ya jiji la Mbeya.Eneo
hili ndipo yanapofanyika maadhimisho ya sikukuu ya mashujaa,ambapo viongozi wa
serikali,dini na kimila huwa wanakuja kuweka mashada ya maua na kuwaombea
mashujaa wetu wa Tanzania waliopoteza maisha yao kwa ajili ya kuitetea na
kuilinda nchi yetu ya Tanzania

sawa kaka
ReplyDelete