Tuesday, 20 August 2013

  “   THE TALENTED”
Uhuru selemani
  imeandikwa na Abdul "be good"Sudi/picha kwa hisani ya uhuru selemani.



       Mmoja kati ya wachezaji wenye vipaji halisi hapa Tanzania ni Uhuru Selemani,kwani pamoja na misuko suko ya majeruhi iliyokua ikimkabili lakini kila akiingia uwanjani anaonyesha kiwango kile kile alichokua nacho kabla ya kuumia.Na sasa hivi ,yupo vizuri  zaidi ya alivyokua misimu iliyopita. “namshukuru Mungu sasa hivi nipo salama,sina tatizo tena na naomba uzima nitaonyesha kiwango kikubwa zaidi ya nilichoonyesha kabla”alinambia Uhuru ambae kwa sasa yupo Coastal Union akitokea klabu ya SImba aliyokua nayo msimu uliopita. “unajua ukiwa majeruhi wa mara kwa mara hata wewe mwenyewe unachanganyikiwa,unakua hujiamini,uoga wa kuumia unakufanya usicheze kwa uhuru unaoutaka,lakini kwa sasa niko vizuri mno na naamini nitaonyesha kiwango changu halisi”
         Uhuru ana uwezo wa kucheza namba nyingi uwanjani,kwani pamoja na mara kwa mara kuchezeshwa kama kiungo wa pembeni lakini ana uwezo wa kusimama kama mshambuliaji na hata  kucheza kama kiungo wa juu.na kama lilivyo jina lake yupo huru sana akiwa na mpira kiasi ana uwezo wa kupiga chenga huku anakwenda mbele na pia ana uwezo wa kupiga miguu yote hivyo inakua ni ngmu sana kwa mabeki kumkaba akiwa na mpira,wanakuwa hawajui ataufanya nini mpira,na hata ukitazama magoli anayofunga ni ya uhakika si ya kubahatisha,kwa vile ana kipaji halisi.ni wachezaji wachache sana wenye uwezo wa kkupiga mashuti huku wanakimbia,lakini Uhuru anafanya hivyo mara kwa mara…

    Uhuru Selemani alizaliwa mkoani Mbeya katika wilaya ya Mbarali na alianza elimu yake ya awali katika shule ya  msingi Mbarali na kuja kumalizia Kawe Dar es salaam “toka nikiwa shule ya msingi nilipenda kucheza mpira,kiasi nilipokua mkubwa kidogo nikajiunga na wenzangu katika timu ya Ibara kids,pale tumecheza sana kisha baadae nikachukuliwa na rujewa kids zote za Mbeya na hata nilipohamia Dar moja kwa moja nikajiunga na ukwamani kids yak awe,,na huko tukawa tunafanya vitu vikubwa kiasi tukapata mashabiki wengi sana….unajua nimecheza mashindano ya muungano Mufindi nikiwa na umri mdogo sana lakini nilikubalika kwa vile kiwango changu kilikua ni cha uhakika”
     Uhuru amewahi kuchezea timu kadhaa ikiwemo Mtibwa,Coast,Azama ,na Simba  ana uzoefu wa kucheza katika hali  yoyote “Ninashukuru nimeanza kucheza mpira wa ushindani nikiwa mdogo sana hilo limenikomaza na kuweza kupambana na changamoto za kila aina,kila timu unayokwenda unakuta ina mifumo yake,tokay a uchezaji hadi ufundishaji,hivyo nimepitia mambo mengi sana sasa hvi nishakua mzoefu wa fitna za soka”alinielezea. “Nafurahia sana maisha ndani ya timu yangu ya Coastal Union,kwani hakuna mazengwe ya kutengenezeana,hapa mtu unacheza kutokana na kiwango chako,tofauti na inavyokua kwa timu hizo zinazoonekana ni kongwe hapa Tanzania,kule mwenye sauti ya mwisho nani acheze na nani asicheze si kocha,ni watu tofauti kabisa wenye nguvu za ajabu katika hizo timu,ndio maana utashangaa kila siku wanaacha wachezaji wazuri na kusajili vichekesho,nimepita huko najua naloongea,unafanya mazoezi vizuri,kocha anakufurahia na kukusifu na kukupa matumaini unajua mechi inayokuja unacheza lakini baadae ikitajwa list unakua haupo,kisha unaanza kusikia rumours,kua kuna kiongozi pengine hakupendi au hataki ucheze…unaweza hata kuzushiwa sababu za ajabu…huna nidhamu au lolote na itokee bahati mbaya ukakosea siku uliyopangwa mashabiki wale wale wa timu yako ndio wanakua wa kwanza kukupigia kelele na kumlazimisha kocha akubadili…siwalaumu kwani najua wanakua tayari wameshalishwa sumu”aliongea Uhuru “lakini kwa timu nyingine hali ni tofauti,presha inakua ndogo ndio maana hata mchezaji unakua na amani na unafanya vizuri.

     Uhuru amechaguliwa mara kadhaa kuichezea timu ya Taifa,na mechi ambayo kila mtu anaikumbuka ni siku Tanzania walipocheza na Brazil “kila mtu duniani anatamani kucheza na Brazil,nashukuru mumngu nilipata nafasi ya kucheza na wachezaji bora kabisa duniani,mara nyingi unawaona katika tv lakini nimebahatika kucheza nao…fikiria unacheza na mchezaji unaempenda kama Robinho,unakabwa na mchezaji kama Dani Alves,hiyo ni kumbukumbu nitakayobaki nayo hadi nakufa maana si wote wenye bahati kama yangu”

   Kwa sasa Uhuru amesajiliwa na timu ya Coastal Union ya Tanga akitokea timu ya Simba.na kwa matayarisho aliyoyafanya ana uhakika wa kucheza vizuri zaidi  msimu huu….tuko pamoja HOME BOY……

No comments:

Post a Comment