Tuesday, 17 September 2013

 MBEYA CITY
 Tumaini la          soka Mbeya
            IMEANDKWA NA ABDUL "be good"SUDI.MBEYA

                                                                   
                                                    SEHEMU YA MASHABIKI WA MBEYA CITY
Miaka kadhaa iliyopita mkoa wa Mbeya ulikua ukisifika kwa kutoa wachezaji wazuri na wengi waliokuwa wakienda kuchezea timu mbali mbali kubwa za hapa nchini,Kuanzia kina Rajab Muhoza na Mtawa Kaparata waliokwenda kuchezea Maji Maji ya Songea kwa vipindi tofauti,kina Justin Mtekere,Salum Kabunda,Sekilojo Chambua,Suleiman Mathew,Godwin Aswile,Mbwana Makata na Steven Mussa waliokwenda Yanga na kua ni wachezaji maarufu sana nchini,kina Aston Pardon,Michael Kidilu,Maumba Mikidadi waliokwenda Simba na wengine wengi waliokwenda timu tofauti kutoka mkoani Mbeya.Na hilo lilitokana  na kuwa kulikua na uongozi imara wa chama  cha soka mkoani  Mbeya uliokua ukiongozwa na mwenyekiti marehemu mzee Aban Nusura uliokua umesimama imara kuhakikishaTukuyu Strars inapanda daraja toka daraja la tatu hadi kua bingwa wa Tanzania na timu tishio sana hapa Tanzania, ilikua si ajabu timu kubwa kutoka Malawi au Zambia kuja Mbeya kucheza michezo ya kirafiki,timu kama Nkana Red Devils na Mufulira wonderers zilikua zikija mara kwa mara na kuna mwaka hata timu kutoka Denmark ilikuja na kuonyesha burudani safi sana kwa wakazi wa Mbeya.Hizo zote zilikua ni changamoto kwa timu za Mbeya za wakati ule ili kuzipa mazoezi na uzoefuwa kucheza michezo mikubwa.Na mafanikio yalionekana kwani timu kama Tukuyu Stars ikafanikiwa kupanda daraja hadi kuchukuaa ubingwa.
Mashabiki wa mkoa wa Mbeya wana nafasi kubwa sana kwa mafanikio ya timu hiyo ya Tukuyu Stars na hata Mecco,kwani wakazi wa Mbeya wana sifa ya kupenda timu zao,na mar azote hua wanazipa sapoti ya asilimia kubwa sana,ni nadra sana kukuta mtu wa Mbeya aliyezaliwa Mbeya akiishanglia timu toka nje,mara nyingi wanaoshangilia timu pinzani wanakua ni watu wa kuja si wazawa wa Mbeya.Ndio maana hata timu ya Prison mwanzo ilikua na mashabiki wengi sana  lakini hali ikabadilika baada ya uongozi kuamua kusajili wachezaji wengi toka katika magereza morogoro na kuacha vijana wengi toka mkoani Mbeya hivyo wakazi wa Mbeya wakaona kama wamesalitiwa na kuamua kuacha kuisapoti timu hiyo.Ingawa sasa hivi hali imebadilika baada ya kuamua tena kuisapoti timu hiyo na ni baada ya kusajili tena wachezaji wengi toka mkoani mbeya.
   Sasa hivi imekuja timu kipenzi cha wakazi wa Mbeya,timu ya MBEYA CITY,timu ambayo imepanda daraja msimu huu na kua inacheza katika ligi kuu ya  Tanzania.Kutokana na usajili wake ulivyokua mzuri na jinsi walivyofanikiwa kupanda daraja kabla hata ligi haijaisha,kumewafanya wakazi wa mbeya kua na imani kubwa sana na timu hiyo.na hata katika mech zao za mwanzo imeonyesha ina dhamira ya kushindana si kuwa msindikizaji.nilipoongea na baadhi ya wakazi wa Mbeya kusu timu hiyo,hawakusita kueleza furaha na mapenzi wwaliokua nayo kwa timu hiyo,na wengi walieleza matumaini ya kuja kua ni moja kat ya timu bora sana hapa Tanzania.Nilipotembelea eneo maarufu kwa biashara eneo la Mwanjelwa nilikutana na mfanya biashara wa nguo ambae alikua akiuza jezi za timu ya Mbeya City,mfanyabiasahara huyo aitwae FESTO DOMNGO  alinambia “hii ni timu halisi ya mkoa wa Mbeya kwani hata wachezaji wengi waliosajiliwa ni wa hapa hapa Mbeya,hivyo tunawajua  toka wanaanza kucheza mpira na tulikua tunawafatilia na kuwaona ni wazuri sasa wamesajiliwa na timu ya hapa mkoani sina budi kuishangilia na kuona ni yetu kabisa wakazi wa Mbeya,ninaipa sapoti kwa asilimia mia”alinambia huku akiibusu jezi yake aliyovaa ya Mbeya City.

                                                     FESTO DOMINGO
 

                                                                                   JOSEPHAT MWAKALEKANE
Shabik mwingine aliyejulikana kwa jina la AMBWENE MWAKALOBE yeye alisisitiza tu kua “ninaiamini sana timu ya MBEYA  CITY,huyu ndio mkombozi wa soka la Mbeya kwani wanajituma sana na wachezaji wana nidhamu hata ukiwatazama mazoezini unaona wana dhamira ya kufika mbali,ninawaommbea kwa mungu wafanikiwe na kuutoa kimasomaso mkoa wetu wa Mbeya”

                                             AMBWENE  MWAKALOBE
Hata niliotembelea eneo la kabwe katika sehemu ambayo ina maduka ya kuuza viatu,hapo nilikutana na mashabiki wengine waaliokua wamevaa jezi za MBEYA CITY,na niliongea nao na wakawa na haya ya kusema. “wakazi wa Mbeya tunapenda sana soka,na kila mara mkoa unakua na wachezaji wengi sana maana hata ukitazama kuna mashindano mengi sana yasio rasmi yanayoendeshwa hapa mkoani,na ukitazama vwango vinavyoonyeshwa na hao vijana ni vya hali ya juu sana ndio maana hatujashangaa kuona timu ya MBEYA CITY ikichukua wachezaji wengi toka hapa hapa mkoani,na mimi ni mkazi wa Mbeya lazima niipende timu yangu,naona rah asana kuwatazama madogo wa mtaani wakiichezea timu ya nyumbani”alinieleza FRANK MWAMBENE mfanyabiashara wa viatu hapo sokoni kabwe.


                                                                                                FRANK MWAMBENE

No comments:

Post a Comment