ADNAN JANUZAJ
KINDA LA MAN UTD
Adnan
Januzaj amecheza mechi moja tu kamili
toka ajiunge na timu ya Manchester United,lakini nchi tano zote zinataka
akachezee timu zao za taifa.Nchi za Uturuki,Serbia,Kosovo na Albania pamoja na
nchi aliyozaliwa ya Ubelgiji zote zinataka azichezee,na hata Uingereza nao
wameanza kampeni za chini chini za
kutaka kumchukua ili awe raia wa nchi yao.
Januzaj
alizaliwa Ubelgiji,ingawa wazazi wake walitokea Albania,ingawa nao kwao ni Kosovo.na
walikuwa wamekimbia vita hivyo wakapata uraia wa Ubelgiji.
Alichukuliwa
na timu ya Anderlecht ya ubelgiji alipokua na miaka 10 na akakaa hapo hadi
alipofikisha miaka 16 ndipo akachukuliwa na Manchester United.Wakati kocha wa
zamani wa Manchester United anataka kujiuzulu alimkabidhi Januza jezi namba
44.Mechi yake ya kwanza ilikua ni katika kombe la ngao ya hisani dhidi ya Wigan
alipoingia badala ya Van Persie,nay a pili alimbadili Ashley Young walipocheza
na Crystal Palace,na mechi ya tatu
ambayo alianza toka mwanzo ni walipocheza na Sunderland na akafanikiwa kufunga
magoli yote mawili waliposhinda 2-1.
Ni mchezaji
mwenye kasi,anaetumia sana mguu wa kushoto,anapiga chenga na anajua kufunga.alifanya
vizuri sana wakati wa michezo ya majaribio kabla ya kuanza kwa msimu huu,na
ingawa bado ana umri mdogo wa miaka 18 tayari kishaonyesha atakua ni mmoja kati
ya wachezaji wazuri sana duniani.
Ingawa nchi zote hizo zinataka akachezee timu zao
za taifa lakini mwenyewe bado hajaamua akacheze wapi,lakini baba yake anasema
atafurahia sana kama akiichezea nchi ya Albania.



No comments:
Post a Comment