MBEYA CITY KUCHEZA NA RHINO
MBEYA CITY FC
Timu ya
Mbeya City leo inacheza na timu ya Rhino ya Tabora katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara,mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini
Tabora.Akiongea na Mbeya Maskan kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi amesema timu katika hali nzuri,na
wanatarajia mchezo utakua mgumu na mzuri kwani wanaiheshimu Rhino kwa jinsi wanavyocheza
lakini wamejitayarisha vizuri kukabiliana nao,na mungu akipenda atashnda.Hadi sasa Mbeya City imecheza
mechi tatu ugenini,dhidi ya Mtibwa wakatoka sare ya 0-0,kisha wakacheza na
Simba pia wakatoa sare ya 2-2 kabla hawajacheza na Oljoro na kuifunga 1-0.Mbeya
City wamepania kushambulia sana katika mchezo wa leo,kwani wanahitaji point
tatu ili wazidi kusogea juu zaidi katika msmamo wa ligi kuu.Mbeya City
wanashika nafasi ya 11 wakiwa na point 11,wakishinda leo watapishana kwa pointi
moja na kinara wa ligi hiyo Simba wenye pointi 15.
KIKOSI CHA
MBEYA CITY LEO KITAKUA
1.David
Baruan
2.John
Kabanda
3.Hassan
Mwasapile
4.Deo Julius
5.Anthony
Mayunga
6.Yusuph
Abdallah
7.Alex Setth
8.Steven
Mazanda
9.Paul Nonga
10.Jeremiah
John
11Deus
Kaseke.
KILA LA
KHERI MBEYA CITY.

No comments:
Post a Comment