Thursday, 3 October 2013

tatizo nini
MAN UNITED?

                               imeandikwa na Abdul(be good) Sudi,Mbeya
Kabla hajajiuzulu,aliyekua kocha wa Manchester united,sir Alex Ferguson alisema ameiacha timu ikiwa katia kiwango cha juu sana,lakini toka aje David Moyes kikosi kimebaki kile kile,lakini had sasa baada ya michezo sita imeejikuta iko katika nafasi ya 12,nafasi ya chini kuwahi kufika kwa muda mrefu sana.toka mwaka 1989.
Tatizo ni nini??hiki ndio kikosi kilichochukua ubingwa ligi kuu msimu uliopita,je tatizo n wachezaji wamechoka au tatizo liko kwa kocha David Moyes??
Ukitazama sana toka msimu uliopita timu ilionyesha kwamba inahitaji viungo,lakini hadi dakika za mwisho wakati dirisha la usajili linataka kufungwa ndio akasajiiwa Marouane  Fellaini,hivyo hajapata muda wa kukaa sana na wenzake kabla ligi hajaanza kucheza,hvyo bado anahitaji muda wa kuchanganya.
 Wachezaji wakongwe kama Ryan Gigs,Rio Ferdinand,Nemanja Vidic na hata Carrick wanashidwa kwenda na kasi ya mchezo hivyo inawapa shida sana pale wanapokutana na timu zinazojua kufanya mashambulizi ya kushtukiza “counter attack,

Kuna tatizo la majeruhi wanaotokea mara kwa mara,kama ilivyotokea kwa Rafael da Silva na kuwafanya wachezaji kama Phil Jones na Chris Smalling kupangwa pembeni hivyo kwa vile hawana mazoea ya kucheza nafasi hiyo timu inashindwa kushambulia na silaha kubwa sana kwa man ni kushambulia toka pembeni.

Na kikubwa kinachowasumbua mashabiki ni kwa nini hamchezeshi Shinji Kagawa kama kiungo wa juu,kwani alipokua Borusia Dotmund alikua akiicheza nafasi hiyo na kufunga magoli mengi mno na kutoa pasi nyingi za magoli,lakini hakuna anaeelewa kwa nini Moyes hamuamini,na hata akimpanga anamuweka nafasi ambayo si yake,pembeni kitu kinachofanya ashindwe kucheza vizuri.inashangaza kuona timu inasumbuliwa katika kiungo wakati katika benchi kuna kiungo wa kiwango cha juu.
UPANDE wa pembeni Luis Nani peke yake ndio anacheza kwa kiwango cha juu,lakini Ashley Young bado hajaonyesha kama ana sifa ya kua ni mchezaji wa timu kubwa kama ya Manchester United,na hata  Valencia sio Yule wa misimu miwili iliyopita bado hajaonyesha makali yake hivyo timu inashindwa kupata mipira ya kutokea pembeni kama ilivyokua misimu iliyopita,angalau upande wa Evra ndio anaweza kuleta  pasi kadhaa za magoli.

Ukitazama kwa makini ,kocha ana sababu nyingi sana za kulaumiwa kwani alipochukua nafasi,ilitakiwa abaki kwanza na wasaidizi wa Ferguson katika benchi la ufundi  ili wamuonyeshe njia lakini akaamua kuleta watu wapya ambao hadi sasa inaonekana wanashindwa kumshauri vizuri,ndio maana timu inasumbuka na anashindwa hata kuibadili,ikumbukwe wakati wa ferguson alikua akiweza kuubadili mchezo katika dakika 15 za mwisho,na hakuna siku hata moja Manchester iliwahi kuelemewa mwanzo hadi mwisho, ukiondoa walipocheza na Barcelona,lakini sasa hivi kila ikicheza mashabiki wake wanakua na wasiwasi,maana wanakua hawana uhakika wa ushindi.

No comments:

Post a Comment