MBEYA CITY KUWAVAA OLJORO JKT
NA
ABDUL SUDI.
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania inaendelea jumamosi hii kwa timu ya Mbeya City,kucheza na timu ya JKT
Oljoro katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeid Arusha katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kuvutia.Timu ya JKT
Oljoro ipo katika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi baada ya kushinda mechi
moja na kutoa sare michezo miwili na kupoteza mitatu,wakati timu ya Mbeya City
inashika nafasi ya nane ikiwa na point 8 baada ya kushinda mchezo mmoja na
kutoka sare michezo mitano.
Kocha wa timu ya Mbeya City Juma Mwambusi amesema kikosi kipo katka hali nzuri na
anategemea ushindi katika mchezo wa leo,anasema hana wasiwasi na majeruhi kwani
timu yake inacheza kitimu zaidi ya kumtegemea mtu mmoja mmoja “wachezaji wa
Mbeya City wote wapo katika kiwango sawa,kwa vile wanacheza kitimu,hatumtegemei
mchezaji mmoja mmoja ndio maana utaona hata nikifanya mabadiliko anaeingia
anakua na uwezo ule ule kama wa yule aliyetoka,hivyo inakua rahisi kuunganisha
na wenzake”.alisema alisema kocha
Mwambusi.
KILA
LA HERI MBEYA CITY

No comments:
Post a Comment