Sunday, 6 October 2013

Tz Prison yaifunga Mgambo shooting 1-0

                                                             Tz prison
Timu ya TZ PRISON imefanikiwa kupata ushindi muhimu wa ugenini dhidi  ya timu ya Mgambo Shooting  ya Tanga katika mchezo mzuri uliochezwa katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.Katika mchezo huo Tz Prison  ilitawala sana kipindi cha kwanza na kufanikiwa kulisakama  mno goli la Mgambo,lakini uhodari wa mabeki uliwasaidia kutokufungwa mapema.hadi kipindi cha kwanza kinakwisha  hakuna timu iliyo fanikiwa kupata bao.

Tz Prison walikianza kipindi cha pili kwa nguvu zaidi na kufanikiwa  kupata goli katika dakika ya 65 baada ya kazi nzuri ya Julius Hamisi aliyekimbia na mpira na kupiga krosi nzuri iliyomkuta  Peter Michael aliyeukwamisha wavuni.Tz Prison waliendelea kulisakama goli la Mgambo na kukosa nafasi kadhaa.hadi mchezo unakwisha  Tz Prison  waliondoka na ushindi wa goli moja kwa bila.

No comments:

Post a Comment