TZ PRISON
KUWAVAA MGAMBO JKT LEO
IMEANDIKWA NA ABDUL SUDI
KIKOSI CHA TANZANIA PRISON
Timu ya Tz Prison ya Mbeya leo inacheza na timu ya Mgambo JKT katika ligi kuu ya Vodacom
Tanzania bara.mchezo huo utafanyika katika uwanja wa mkwakwani Tanga.Tanzania
Prison inashika nafasi ya 13 ikiwa na point 4 baada ya kufungwa michezo miwili
na ruvu shooting na ruvu jkt,kabla ya kutoka sare michezo minne na timu za coastal union 0-0,Yanga 1-1,Mtibwa 1-1,na pia
kutoka sare na Azam kwa goli 1-1,wakati timu ya Mgambo inashika nafasi ya 12
ikiwa na point 5 baada ya kupoteza mechi mbili walipofungwa na Ruvu Shooting
1-0,kisha wakaja kuaibishwa na Simba 6-0,wakatoa
sare na oljoro 0-0,na Rhino 1-1 na kushinda mechi moja dhidi ya Ashant kwa
kuifunga goli 1-0.
Mchezo huo ni muhimu sana kwa Tz Prison kwani inahitajika
lazima ishinde ili ijiweke katika mazingira mazuri na kuongeza imani kwa
mashabiki wake walioanza kurudi kwa kasi kuisapoti timu hiyo.Kwa mujibu wa
viongozi waliofatana na timu,wachezaji wapo
katika hali nzuri na jana
walifanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa mkwakwani.Wachezaji wote wana ari
na mchezo huo na wamepania kucheza kwa juhudi zote ili wazipate point zote
tatu.
Kikosi cha Tz Prison kitakachoanza leo ni
1.BenoDavid
2.Salum Kimenya
3.Boniface Hau
4.Jumanne Elfadhili
5.Nurdin Issa
6.Jimmy Shoji (GEMMA)
7.Jeremiah Juma
8.Omega Seme
9.Peter Michael
10.Ibrahim Isaka
11.Julius Khamis.
Wachezaji wa akiba ni Albert Mweta,Laurian
Mpalile,Lugano Mwangama,Fredy Chudu,John Matei,Six Mwasekaga.
KILA LA HERI TANZANIA PRISON

No comments:
Post a Comment