YANGA VITANI NA AL AHLY
Yanga ya Tanzania, jumamosi
inakutana na mabingwa wa Misri Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa klabu bingwa
Africa, Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo, Yanga wanatakiwa
kushinda kwa idadi yoyote ya magoli kwani si rahisi kuzifunga katika viwanja vyao, hivyo
inatakiwa Yanga wahakikishe wanapata ushindi mnono hapa hapa nyumbani.
Kikosi cha Yanga kina wachezaji wengi wenye
uzoefu wa michezo mikubwa, kama Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Mrisho Ngasa,
Didier Kavumbagu, Athman Iddi, Hamis Kiiza, na sasa hivi ameongezeka Emanuel
Okwi, hivyo haina haja ya kuogopa timu pinzani.
![]() |
| EMANUEL OKWI |
Yanga wana washambuliaji wakali sana
lakini ina mapungufu katika ulinzi ambayo nina uhakika hadi sasa kocha tayari
atakua ameyafanyia kazi, tatizo dogo lililopo kwa timu hiyo ni kwamba hawana
beki wazuri wa pembeni kwani Oscar Joshua na Mbuyu Twite katika siku za
karibuni hawako katika viwango vizuri, lakini kama wakituliza akili wana uwezo
mkubwa sana wa kuwazuia Ahly.
Timu ya Al Ahly inategemewa kucheza
mchezo wa jumamosi kama wanavyocheza katika michezo mingi wakiwa ugenini,
wanaulinda sana mpira na kupiga pasi nyingi sana ili kuwapoza na kuwafanya mjisahau kisha hua
wanashambulia kwa haraka sana na mara nyingi anaeanzisha mashambulizi anakua ni
beki wa pembeni, hivyo Yanga wawe makini sana na aina hiyo ya uchezaji.
![]() |
| AL AHLY WAKIWA MAZOEZINI IST |
Lakini kwa Yanga timu yao ina washambuliaji wote wenye kasi sana, nan i rahisi
wakipata nafasi kuzitumia. Mchezaji kama Simon Msuva kwa sasa hivi yuko katika
kiwango cha juu sana hivyo anatarajiwa kuwapelekea mipra mara kwa mara kina
Okwi na Kavumbagu ili wapachike magoli.
Mungu ibariki Yanga ishinde.



No comments:
Post a Comment