yanga
yawaduwaza al alhly
Klabu bingwa ya Tanzania Yanga,
leo imevunja mwiko baada ya kuwafunga Al Ahly yaa Misri goli moja kwa bila
katika mchezo wa klabu bingwa Afrika. Toka waanze kukutana mwaka 1982, hii ni mara ya kwanza kwa Yanga kushinda.
Nahodha wa Yanga Nadir Haroub
aliipatia timu yake goli hilo muhimu dakika nane kabla mchezo huo haujamalizika.
Katika mchezo huo Yanga waliutawala kwa
kipindi kirefu ambapo Mrisho Ngasa, Emanuel Okwi, Simon Msuva na Hamisi Kiiza
walikua wakiwasumbua muda mrefu walinzi wa Al Ahly.
![]() |
| MASHBIKI WA YANGA WAKIWA WAMEKAA UPANDE WA SIMBA |
Simon Msuva alikaribia kufunga katika dakika ya 18 lakini
mpira aliopiga uliokolewa kiufundi na kipa wa Ahly, dakika moja baadae Emanuel Okwi nae alipiga
kichwa kilichookolewa na kipa
Dakika ya 26 Hamisi Kiiza alikosa bao la
wazi baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Msuva lakini akaupiga mpira uliotoka
nje.
Ingawa hatari hazikua nyingi upande wa Yanga, lakini walinzi wake
walicheza vizuri sana katika mchezo huo hasa nahodha wao Haroub alieza kuwainda vema washambuliaji wa
Ahly wasilete madhara.
Goli la Yanga lilipatikana baada ya
juhudi za mshambuliaji wake Emanuel Okwi aliyeingia na mpira katika eneo la
hatari ndipo walinzi wa Ahly waautoa ikawa kona, na Msuva akapiga kona nzuri
iliyomkuta Nadir Harou aliyepiga kichwa kifundi na mpira ukamshinakipa wa Al
Ahly Sherif Ekramy na kuingia golini.
Al Ahly waliwachezesha washambuliaji wawili, Mohamed Nagy "Gedo"na Amr Gamal huku wakimuanzisha kiungo wake mpya toka Burkina Faso Musa Yedan lakini hawakua na mipango mizuri ya kuipenya ngome ya Yanga iliyoongozwa na Nadir Haroub ambae alicheza vizuri sana katika mchezo huo.
Katika mchezo huo Yanga walionyesha kiwango cha hali ya juu na walikua wakifanya mashambulizi yenye mpngilio lakini uimara wa walinzi wa Ahly uliwafanya washindwe kupenya na kufunga magoli mengi.
Mchezo wa marudiano utafanyika jumapili ijayo jijini Cairo.




No comments:
Post a Comment