Mamia ya mashabiki wa Mbeya City, walisafiri toka jijini Mbeya kuifuata timu yao ilipokua
ikicheza na JKT Ruvu(ruvu stars)katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini
Dar.
Kama
ilivyokua kwa michezo mingi, timu yao haikuwaangusha
mashabiki wake, kwani ilishinda kwa magoli mawili kwa bila, magoli yote
yakipachikwa na mmoja kati ya washambuliaji wake hatari Saad Kipanga.
Magoli
hayo aliyafunga moja kila kipindi,
lakini yote mawili kwa mashuti. La kwanza alilifunga dakika ya
tisa baada ya kukutana na mpira wa Mwegane Yeya uliookolewa na mabeki baada ya
shambulizi kali na kumkuta mfungaji aliyepiga fataki kali llilomshinda kipa
mzoefu wa JKT Shaaban Dihile.
La pili
lilikua zuri zaidi, kwani baada ya JKT kushambulia kwa nguvu ili kutafuta bao la kusawazisha,
walijisahau nyuma na mpira mrefu uliopigwa
na mabeki wa City ulimkuta Paul Nonga aliyekua peke yake na mabeki wa
JKT, aliutuliza mpira na kuwasubiri wenzake kisha akampasia Mwegane nae
akamuwekea Kipanga aliyepiga shuti kali zaidi la mguu wa kushoto na kutinga moja kwa moja wavuni na kuandika bao
la pili.
City
waliutawala sana mchezo hasa kipindi cha kwanza na walifanya mashambulizi mengi
langoni mwa JKT, na kama wangeku makini zaidi wangeweza kupata ushindi mkubwa
zaidi.
Pamoja na
ushindi huo, lakini burudani ilikua ni kwa mashabiki wake waliokua
wakishangilia kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo huo bila kuchoka.
‘Tunaona
fahari sana kuishangilia timu yetu, inatupa furaha na umoja ambao ni vigumu
sana kuutenganisha” aliongea shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Joe
Mwakatumbula aliyetokea kwa mama John
jijini Mbeya. “nimesafiri kutazama michezo yote ya Mbeya City, ni mmoja tu
niliukosa siku walipocheza na Rhino Tabora, na ilikua ni kwa sababu nilipata
msiba, lakini sijakosa mchezo mwingine wowote wa Mbeya City” aliongeza kwa
furaha.
Nae John Mwakalebela ambae ametokea maeneo ya
Airport alisema “hii ni timu yetu watu wa Mbeya hatuna budi kuipa sapoti kila
tunavyoweza maana inawakilisha vizuri
jiji letu, na kikubwa kinachofurahisha, wanajituma kwa juhudi sana na
kutupa raha tunyoitarajia”alimalizia Mwakalebela.
Pia kulikua na kina dada kadhaa ambapo mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina la Lucy Kalinga alisema " nimesafiri toka Mbeya hadi Dar, lakini nimeridhika na kiwango cha timu na matokeo tuliyopata, kwa sasa nguvu yetu tunaipeleka katika mchezo unaofuata dhidi ya wapinzani wetu wa jadi Tz Prisons, na tuna uhakika wa ushindi, lazima tupate nafasi mbili za juu"alitamba dada Lucy.



.jpg)

No comments:
Post a Comment