Taifa stars sare na Namibia
Timu ya soka ya Taifa Stars ya
Tanzania, wametoka sare na Brave Warriors ya Namibia kwa kufungana goli moja
kwa moja katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Tanzania walikuwa kwanza kupata bao
baada ya beki wa Namibia Emilio Martin wakati wa jitihada za kuokoa alijikuta akiusindikiza wavuni mpira wa kona
iliyopigwa na Mcha Khamisi.
Namibia walisawazisha goli hilo katika
dakika za majeruhi kwa bao lililofungwa na Panduleni Nekundi.
Stars ambayo ilikwenda bila nyota wake wanaochezea timu ya
Yanga na wale wanaocheza mpira wa kulipwa walionyesha mchezo mzuri na wa
ushindani.


No comments:
Post a Comment