Monday, 13 October 2014

STARS YAAMKA

    Hatimaye timu ya Taifa ya Tanzania, iliwafurahisha mashabiki wake baada ya kuifunga timu ya Benin wa magoli 4 kwa 1.
    Nadir Haroub na Amri Kiemba walionyesha uzoefu wao baada ya kufunga goli la kwanza na la pili kabla ya Thomas Ulimwengu kuongeza la tatu na Juma Luizio kumalizia la nne.

   Stephane Sessegnon aliyevaa kitambaa cha unahodha cha Benin alikuwa na wakati mgumu katika mechi hiyo ambayo timu yake wachezaji walipoteana uwanjani.
Nadir Haroub aliwafunga goli la kwanza kwa kichwa kufuatia mpira wa adhabu uliyopigwa na Erasto Nyoni dakika ya 19 ya mchezo.
Baada ya kupata goli hilo Stars waliendelea kucheza vizuri na kuwafanya Benin walioonekana wamechoka toka mwanzo kua na wakati mgumu.
    Amri Kiemba alifunga goli la pili dakika ya 40 akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Mwinyi Kazimoto, ambae jana alicheza vizuri tofauti na michezo mingine iliyopita.
Amri Kiemba akishangilia goli lake


 Dakika nne toka kipindi cha  pili kuanza, Thomas Ulimwengu aliipatia Stars goli la tatu.
Thomas Ulimwengu akimtoka  beki wa Benin
Benin walipoteana zaidi na kuwafanya Stars kutawala sehemu kubwa ya mchezo, na katika dakika ya 72, Juma Luzio aliipatia Stars goli la nne.
 Benin walipata goli lao dakika ya 90 ya mchezo.
Juma Luzio akifunga goli la tatu
  Stars: Mwadin Ali, Shomari Kapombe, Nadir Haroub 'Cannavaro'/ Said Mourad , Erasto Nyoni, Aggrey Morris,Oscar Joshua, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba/ Salum Aboubakar , Haroun Chanongo/ Said Ndemla, Mrisho Ngasa/ Juma Luizio na Thomas Ulimwengu. Khamis Mcha .

Benin: Farnoue Fabien/ Allagbe Saturnin , Tossavi Eric, Ore Fortune, Dabarou Nana, Ogouchi Jean, Adeoti Jordan, Mama Seibou/ Baraze Seidou , Sessegnon Stephane, Pote Mickael, Djigla David/ Suanon Fadel  na Dossou Jodel/ Adoudou Mohammed.

No comments:

Post a Comment