matogoro,mchezaji bora wa mwezi September
Bodi ya ligi kuu ya
Vodacom Tanzania, imemchagua Anton Matogoro waMbeya City kuwa ni mchezaji bora wa ligi hiyo kwa
mwezi September 2014. Amepata na zawadi ya pesa kiasi cha shilingi milioni
moja.
Anton, kiungo wa chini wa timu hiyo, amefanikiwa kuchaguliwa
baada ya kucheza katika michezo miwili ya ligi hiyo, wa kwanza ilikua na JKT
Stars na wa pili ukiwa wa Coastal Union.
Anton ana uwezo mkubwa wa kupiga pasi, ziwe
fupi ndefu na pia anajua sana kuziba nafasi ili kupunguza mashambulizi,
alistahili kuchaguliwa hata katika ligi kuu iliyokwisha, kwani katika mchezo
waliocheza na Azam jijini Dar, alitawala sana sehemu ya kati kati na kuwapa
wakati mgumu viungo wa Azam. Na hata
katika mchezo waliocheza na Yanga jijini Dar,pamoja na kua pungufu baada ya
kuolewa kiungo mwingine Steven Mazanda, bado alimudu kutawala sehemu ya katikati na kufanya awe nyota katika
mchezo huo.

No comments:
Post a Comment