KI MJINI MJINI
![]() |
| MBEYA MJINI (picha kwa hisani ya Haneef Lohaar) |
Ogopa sana kuibiwa au kutapeliwa unapokua mjini, wengi
wanaoibiwa au kutapeliwa ni wale wanaojiona ni wajanja sana na wa mjini sana
kiasi wanajiamini kupita kiasi, wanasahau kwamba hao wezi na matapeli nao maisha
yao ni ya mjini kila siku na wanaishi kwa kazi hiyo hivyo kila mara wanabadili
mbinu na mitindo ya kufanyia kazi, ni sawa na mfanyakazi yeyote anaeenda
kuongeza elimu chuoni,nao pia wana elimu ya mtaani wanayoongeza kila mara
wanaiita “STREET WISE”……na degree yake ni ngumu kupata lakini ukiipata unakua
kweli umefaulu…..
Ninajaribu kuandika mbinu mbali mbali
zinazotumika na wezi au hao matapeli katika kufanikisha kazi zao, ingawa hizo
mbinu zinabadilika mara kwa mara.
1-UKIENDA mjini,
muangalie sana anaekuelekeza upaki gari yako vizuri….. mara nyingi anakuelekeza
kisha unapofunga mlango kwa funguo yeye anakua kaushika mlango mmoja kitasa
kinakua juu hivyo uki lock huo mlango unabaki wazi, UNAPOONDOKA ANAUFUNGUA NA
KUKUIBIA……. Hivyo hakikisha unaitazama milango yote kama imefunga ndio uondoke.
2.-UKIWA na laptop au kitu cha thamani weka katika
buti la gari, usiweke mbele au kwa urahisi zaidi mwambie fundi akutengenezee
sehemu ya kuweka laptop chini ya kiti cha dereva-maana mara nyingi hua
wanachungulia kama kuna laptop au begi lolote na linawapa hamu ya kuvunja
drisha na kuiba
3-USIONE ushamba kuweka alarm hata mbili katika gari
lako kwani ni rahisi sana kufungua milango au kuvunjiwa kioo kidogo cha nyuma
ya gari na kuibiwa kila kilichomo
zikiwemo power window……
(kuna njia
nyngi wanazotumia kuvunja vioo au kufungua milango. Wanaweza kuweka jiwe katika
kigunia na kuvunja husikii kelele, wanaweza kuchukua ile risasi nyeusi ya ndani
ya plug za gari, wanasaga na kuchanganya na maji wakimwagia katka kioo
kinaachia taratibu, au kufungua mlango hua wanachukua mpira mdogo wa tenis
(kitenes)wanaukata katkati, kisha wanauweka katika tundu la funguo mlango wa
mbele, linajaa kabisa hewa kisha wanapiga kwa nguvu lock inafunguka)HIVYO
SULUHISHO NI KUWEKA ALARM MBILI MAANA HAIWEZEKANI KUZIPIGA SHOTI ZOTE MBILI..
4-UKIBEBA laptop barabarani hakikisha unaiweka upande
ambao sio wa barabarani, kwani mara nyngi wanakuja kwa nyuma na gari au piki
piki na kukuvuta beg na kukimbia nalo hivyo ukiweka upande wa pili inakua ngumu……
5- KWA WALE wanaotafuta nyumba au vyumba vya kupanga
mjini, hakikisha dalali akikuonyesha nyumba na mwenye nyumba, nenda kwa jirani
yeyote hapo karibu ndio uulize tena usikubali mara moja, maana wengi hua ni
wajanja na wezi, kwa uhakika ukionyeshwa nyumba ondoka baadae rudi hata katika
duka la jirani ndio uulize tena muhusika ni nani ili ujiridhishe.
6-NA KWA WALE WENZANGU wanaopenda kununua dawa za kuongeza nguvu za
kiume za kienyeji kwa wamasai au kwa yeyote mara nyingi ni za utapeli, kwani
wanalofanya hao wamasai ni kwenda duka
la dawa kisha wananunua vidonge vya kuongeza nguvu(kama electro au Viagra)kwa buku
3 dozi kisha anaisaga na kuchanganya na unga anaojua yeye kua sio sumu kisha
anakuuzia kuanzia buku kumi…..na ukijaribu unaona booonge la mganga NA KUJIONA UNA NGUVU BALAA kumbe umepigwa changa
la macho…………

No comments:
Post a Comment