David
Mwantika

DAVID MWANTIKA
Sifa kubwa ya beki ni kutumia nguvu na akili,kucheza mipira ya juu na kuusoma mchezo.hivyo vyote anavyo David Mwantika,ambae uhodari wake wa kutumia nguvu na akili umemfanya awe mmoja kati ya mabeki wazuri sana hapa Tanzania,ana uwezo wa kupiga miguu yote miwili,anajua sana kukaba,iwe man to man au hata kukaba nafasi,pia ni mzuri sana wa kutazama mashambulizi kabla hayajafika hivyo mara nyingi amekua akiwapanga wachezaji wenzake ili kuziba njia zote na kulifanya lango lao liwe salama.na kikubwa anachowazidi mabeki wengine ni kua ni mzuri sana kucheza mipira ya juu,hivyo ana uhakika wa asilimia nyingi wa kumlinda kipa wake.

MWANTIKA AKIMDHIBITI SAID BAHANUZI WA YANGA
“Kucheza mpira si nguvu peke yake,na
akili ina nafasi yake,hivyo kikubwa kinachotakiwa unapokua uwanjani ni kuwa
makini muda wote wa mchezo,usiondoe mawazo mchezoni hata kwa sekunde moja kwani
unapojisahau hapo hapo watu wanatumia nafasi na kuwaumiza”alinambia nilipoongea
nae. “mifano ipo mingi,mnaweza kua mnacheza na kujiona kama tayari mmewazidi
mmnaocheza nao,mnajiamini na hapo ndio kosa kubwa linapofanyika kwani nao
wanakua wanajipanga wapate nafasi,mkikosea kidogo wanawapiga bao inakua kazi
kuanza kutafuta la kurudisha”Alinifafanulia Mwantika aliyezaliwa mkoani Mbeya
sehemu inayoitwa Ilomba,mbele kidogo ya kitongoji maarufu sana cha MWANJELWA
ambacho kina pilika pilika nyingi mno za biashara.Alisoma elimu ya awali katika
shule ya msingi Ilomba,ambapo ndipo alipoanzia kucheza soka “pale shuleni
kulikua na ushindani sana wa soka,maana kama kukiwa hakuna kipindi kinachofanyika
ni kuchukua mpira na kwenda kiwanjani,na huko ilikua ni mashindano maana timu
mbili ndio zinashindana kila siku,na hakuna inayookubali kushindwa”alinieleza David ambae toka akiwa darasa la nne alikua akiichezea timu ya shule “nimecheza sana mashindano ya umitashumta,na wakati nipo shule nikawa
nachukuliwa na timu moja ya mtaani ikijulikana kama HOME BOYS na huko nilkutana na washikaji
wengi sana wanaojua soka la nguvu,nikawa napambana kupata namba na pale
ilinisaidia sana kwani nilianza kujifunza kuwa nikicheza vibaya
sipangwi,nikawa najituma sana kufanya mazoezi na nikipata nafasi ya kucheza
mechi nafanya kweli”aliniambia huku akitabasamu baada ya kuwakumbuka rafiki
zake aliokua nao HOME BOYS…. “kulikua na mafundi sana pale HOME BOYS bahati
mbaya hawakupata nafasi ya kucheza timu kubwa kwani nawakumbuka rafiki zangu
kina GWAKISA,AMULIKE na hata mdogo wangu aliyeitwa ATU walikua wanajua sana
mpira,ni mazingira mabovu ndio yamesababisha hadi wakapotea”aliongeza kwa
masikitiko.
Wakati akiwa HOME BOYS viongozi wa timu ya kijiweni ya Uyole Mbeya
wakamuona na kumchukua. “KIJWENI nako niliikuta timu ina ushindani sana,lakini
nilipigana hadi nikawa na namba ya kudumu,tukacheza ligi daraja la kwanza
ingawa hatukufanikiwa kupanda lakini ilikua ni timu bora sana nako kulikua na
mafundi ambao kila siku nazidi kushangaa kwa nini hawakuja kucheza ligi
kubwa,mtu kama EZE,MTUMBA na hata MOI walikuwa wanajua sana soka tofauti na
watu wengi naokutana nao huku wanachezea timu kubwa huku viwango vyao ni vya kawaida sana,lakini ndio maisha,kila mtu
na alichopangiwa”akasisitiza.

DAVID MWANTIKA AKIMZUIA FELIX SUNZU WA SIMBA
Alipotoka KIJIWENI akachukuliwa na timu ya POLISI
Mbeya ambako hakukaa sana akaenda PRISON
ya Mbeya ikiwa katika ligi kuu ya Tanzania bara,na huko alifanya sana kazi na
kufanikiwa kua na namba ya kudumu. “kule PRISON timu ilikua nzuri na tulikua tunafanya sana mazoezi hivyo tulikua tupo fit sana,tatizo kubwa mechi za
nyUmbani zilikua zinatusumbua kutokana na mashabiki kugawanyika kila
tunapocheza,inakua kama unacheza ugenini,hadi leo sijui sababu gani watu
walikuwa hawataki tushinde wakati nao ni watu wa Mbeya,siwezi kuwasemea kwani wao
wanajua sana sababu zao”
Baada ya kucheza kwa misimu kadhaa
ndipo alipochukuliwa na AZAM mbako yupo hadi sasa. “hapa AZAM timu imetulia,tuko vizuri sana,hata
ikitokea mechi tumepoteza tunajua ni bahati mbaya lakini kwa vipaji na uwezo
tupo juu ya timu zote za Tanzania,msimu huu unaoanza tuna uhakika wa kufanya
vizuri zaidi ya misimu iliyopita,labda yaanze tena mazengwe ya vilabu
vinavyojiita vikubwa lakini kwa soka tu tuko vizuri mno”alinambia Mwantika
ambae katika mechi ya kombe la shirikisho dhidi ya timu ya AFR ya Morocco alitolewa
kwa kadi nyekundu kwa mazingira ya ajabu sana. “hadi leo nikitazama tape za ile
mechi namshangaa refa kwa nini alinitoa nje maana ile ilikua ni shoulder to
shoulder,nikamzidi nguvu,lakini ajabu nashangaa nikapewa kadi nyekundu,niliumia
sana kwani pale ndipo mechi ilipoishia,maana kabla ya kadi nyekundu tulikua
tumeshawashika……”alinambia Mwantika.

DAVID MWANTIKA AKIMTOA NJIANI MRISHO NGASA
David amepania sana kujituma kwa
bidii zaidi ili waweze kutimiza lengo lao na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa
Tanzania. “kwa jinsi timu yetu ilivyo nzur sasa hivi,na ukichukulia tumeshakaa
muda mrefu pamoja hatuna sababu ya kutufanya tushindwe kuchukua ubingwa”alisema
Mwantika anaemkubali sana mshambuliaji wa timu yake Gaudence Mwaikimba.”tutapigana hadi dakika ya
mwisho najua tutashinda”alimalizia …Huyu ndio David Mwantika……HOME BOY aliyepigana kutoka Ilomba
Mwanjelwa Mbeya hadi AZAM FC,na bado safari inaendelea....……



MWANZO MZURI VERY GOOD GUYS
ReplyDelete