Wednesday, 9 October 2013

AMSHA AMSHA MBEYA CITY……
Waichapa Rhino 3-1


Timu ya Mbeya City imefanikiwa kupata ushindi mzuri ugenini baada ya kuifunga timu ngumu ya Rhino ya Tabora magoli matatu kwa moja katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom  uliochezwa katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora.Katika mchezo huo Mbeya City walianza kwa kasi na kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa Rhino lakini umahiri wa golikipa wa Rhino uliwazuia washambuliaji wa Mbeya City kupata magoli mengi.magoli ya mbeya City yalifungwa na Jeremiah Juma,Alex Setth na la tatu likafungwa na Peter Mapunda. Na katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Azam wamefanikiwa kuifunga Mgambo Shooting kwa magoli  2-0, magoli ya Azam yalifungwa na mchezaji aliyepandishwa katika kikosi hicho Farid Maliki katika dakika ya 67 kufuata pasi nzuri aliyopewa na  Erasto Nyoni,na goli la pili lillifungwa na  Kipre Tcheche kwa njia ya penati baada ya mshambulia ji wa Azam Farid kuangushwa ndani ya kumi na nane.Nayo timu ya Mtibwa imewafunga Ruvu JKT kwa magoli 2-1,kwa magoli ya haraka haraka yaliyofungwa na Juma Luzio dakika ya 3 ya mchezo baada ya kazi nzuri ya mkongwe Shaaban Kisiga kuwapunguza mabeki wa JKT na kumpa pasi mfungaji,goli la pili lilipatikana dakika mbili baadae baada ya Mtibwa kufanya shambulizi kali langoni mwa JKT na Juma Luzio akafunga baada ya kupata pasi toka kwa Abdallah Juma.goli la JKT lilifungwa na Salum Machaku baada ya kupiga kona iliyokwenda moja kwa moja wavuni. Nayo JKT oljoro imetoka sare ya magoli 2-2 dhidi ya Ruvu Shooting.    

No comments:

Post a Comment