TZ PRISON KUWAVAA SIMBA
TZ PRISON
Timu ya TZ
Prison ya mbeya jumamosi inakutana na Simba katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.Katika mchezo huo Tz Prison
wataingia huku wakiwa tayari na kumbukumbu ya kuwafunga timu ya Mgambo shooting katka mechi yao ya mwisho
huku Simba wakitoka sare na timu ya Ruvu shooting.Mechi hiyo inatarajiwa kua
ngumu kwani timu ya Tz Prison katika mechi za karibuni imeonyesha kiwango
kizuri tofauti na ilipokanza ligi,wakati Simba kila siku kiwango kinazidi
kushuka hivyo kwa kiasi kikubwa Tz
Prison wanajiamini na wana uhakika wa kupata point zote tatu.Katika
mechi tatu za mwisho timu ya Tz prison ilitoka sare mbili na Azam na Mtibwa
kabla hawajawafunga Mgambo 1-0,wakat Simba ilitoka sare ya 2-2 na Mbeya City
kisha ikaifunga Ruvu JKT 2-0 kabla haijatoka sare tena na Ruvu shooting kwa
goli 1-1.Lakini imekua ikilalamikiwa sana na mashabiki wake kutokana na kiwango
cha chini inachokionyesha pamoja na kushinda.,Mechi nyingine itakayochezwa
kesho itawakutanisha Kagera Sugar na Yanga mjini Kagera.
KILA LA HERI TZ
PRISON

No comments:
Post a Comment