Arsenal yaifunga palace
Arsenal wameweza kufanikiwa
kutanua uongozi wao baada ya kuwafunga Crystal Palace kwa magoli 2-0, moja kwa njia ya penati na Mikel Arteta katika dakika ya 47 baada ya Sergei Gnagby kuchezewa faulo katika
eneo la hatari, na la pili likafungwa na
Olivier Giroud katika dakika ya 87
kufutia krosi safi ya Aaron Ramsey.
Matheu Flamini na Santi Carzola walirudi
kutoka majeruhi ingawa Flamini alimudu kucheza wa dakika 10 tu na kutoka baada
ya kuanza kuchechemea, nafasi yake
ikachukuliwa na Gnabry.
Arsenal walitengeneza nafasi nyingi na
wakafanikiwa kupata goli dakika
mbili baada ya mapumziko baada ya Gnabry kuangushwa na Guedioura na Arteta
kufunga kwa penati.
Dakika ya 65 Arteta alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumvuta Maroune
Charmakh aliyekua akienda kumuona golikipa, baada ya hapo hali ya mchezo
ikabadilika kwani Palace walianza kushambulia na kutafuta goli la kusawazisha,lakini
kipa wa Arsenal Szczesny aliokoa mpira
wa Joe Ward uliokua ukienda pembeni mwa goli na baadae akaokoa tena mpira
uliopigwa na Mile Jedinaks.
Olivier Giroud akaihakikishia Arsenal
ushindi baada a kuunganisha krosi iliyopigwa na Ramsey na kumaliza ndoto za
Palace za kusawazisha.
Kwa ushindi huo Arsenal wamefikisha pointi
22 na kuzidi kujichimbia kileleni wakifuatiwa na Chelsea wenye point 17.




No comments:
Post a Comment