toure ataka waafrika kususia kombe la dunia
Kiungo wa Manchestar City na Ivory
Coast Yaya Toure amesema endapo UEFA
hawataichukulia hatua zinazostahili timu ya CSKA Moscow,nchi za Africa
huenda zikasusia kombe la dunia la mwaka 2018 litakalofanyika Urusi. Toure aliyasema
hayo mara baada ya viongozi wa soka nchini Urusi kukana kwamba hakukua na tukio
la kumdhalilisha Toure au mchezaji yeyote mwenye asili ya Africa jambo ambalo
limepingwa vikali na kiungo huyo. “mimi
sio kiziwi na mara kadhaa nilimwambia mwamuzi
kuwa natukanwa lakini hakuchukua uamuzi wowote kuzuia hali hiyo”alisema Toure.
![]() |
| WACHEZAJI WAKIMTULIZA TORE |
Hivi karibuni shirikisho la
soka ulimwenguni lilitangaza hatua za kuchukuliwa endapo hali kama hii itatokea na ikaamuliwa
mwamuzi analazimika kumaliza mchezo pindi akisikia udhalilishaji kama huo.Raisi wa UEFA Michel
Platini anasema anashangaa kwa nini mwamuzi kutoka Romania Ovidiu Hategan
hakusimamisha mchezo hali hiyo ilipojitokeza na kusema uchunguzi tayari umeanza
kufanyika na hatua kali zitachukuliwa kwa timu hiyo ya Urusi.
![]() |
| YAYA TOURE |
Kumekua na ongezeko kubwa la
udhalilishaji wa waafrika na hali inazidi kua mbaya kwani adhabu zinazotolewa
zinakua ni ndogo sana kufananisha na kosa lenyewe. Klabu zinakua zinatozwa
faini ndogo kiasi inakua kama vile hawajaadhibiwa.
Katika hali ya kushangaza,mchezaji anayechezea
timu hiyo ya CSKA Moscow na raia wa
Ivory Coast kama toure, Seydou Doumbia mwanzo alikaririwa akisema hakusikia milio
kama ya nyani au matusi yoyote yakielekezwa kwa Toure au mwafrika yeyote,lakini
baadae alikana akasema hajawahi kuongea na mwandishi yeyote juu ya jambo hilo
kwa hiyo hajasema hayo maneno.Yaya Toure kwa upande wake alisema anamuheshimu
sana Doumba na anajua kama aliyasema hayo maneno ni kwa sababu ya kulazimishwa
na klabu yake na sio kutoka moyoni.Mchezaji mwenzake wa Manchester City Fernandinho
alisema kama hali hii itaendelea na yeye atakua sambamba na waafrika kususia
kombe la dunia litakalofanyika
Urusi,kwani ni jambo lisilopendeza na linakera.
![]() |
| SEYDOU DEMBA |
Nae kocha wa Chelsea Jose Mourinho
amesema kususia sio suluhisho kwani wanaofanya hivyo ni wachache sana na wanaopinga
ni wengi ni bora zikachukuliwa hatua za haraka ili kuokoa, kwani
kombe la dunia bila waafrika litakua si kombe la dunia tena hivyo
haitakiwi wakasusa bali hatua zichukuliwe haraka kukomesha hali hiyo.




No comments:
Post a Comment