Saturday, 26 October 2013

Man utd
yashinda kwa tabu

                     Man united wamefunga magoli mawili ya haraka haraka na kunusurika na kipigo toka kwa Stoke City waliokua wakiongoza kwa magoli 2-1 hadi zikiwa zimesalia dakika 12,lakini magoli ya Rooney na Chicharito yalisaidia kupata ushindi huo.
PETER CROWCH AKISHANGILIA GOLI LA KWANZA
                  Stoke City walikua wa kwanza kupata goli katika dakika ya nne tu baada ya kipa wa  United De Gea  kuokoa mpira  uliopigwa na Peter Crowch lakini wakati Evans akijaribu kuosha ukamgonga tena Crowch na kuandika goli la kwanza.

                   De Gea alikua tena shujaa baada ya kuokoa michomo kadhaa kabla ya dakika ya  44 Robin Van Persie hajasawazisha kutokana na kichwa kilichopigwa na Wayne Rooney kuokolewa na Asmir Begovic na kumkuta  Van Persie aliyeukwamisha wavuni.
VAN PERSIE AKISHANGILIA GOLI  LA KUSAWAZISHA
                      Lakini  kabla hawajatulia, Stoke wakaongeza goli  kwa faulo iliyopigwa na Marko Arnautovic na kufanya timu hizo kwenda mapumziko Stoke ikaenda kifua mbele kwa magoli 2-1.
MARKO ARNAUTOVIC AKIFUNGA KWA FAULO GOLI LA PILI
                   Man wakashambulia sana kipindi cha pili,hasa alipoingia Adnan Januzaj kuchukua nafasi ya Nani, alibadilisha kabisa hali ya mchezo kwani waliwasumbua vilivyo Stoke na kufanikiwa kusawazisha zikiwa zimesalia dakika 12 baada ya kona ya Van Persie kumkuta  Wayne Rooney akaukwamisha wavuni.
ROONEY AKISAWAZISHA GOLI LA PILI

                  Dakika mbili baadae Chicharito aliyeinga kipindi cha pili kuchukua nafasi ya cleverly alimalizia vizuri krosi iliyopigwa na Patrice Evra na kuandika bao la tatu na la ushindi.
CHICHARITO AKIFUNGA GOLI LA TATU NA LA USHINDI
                 Mabadiliko yaliyofanywa na Man United ya kuwaingiza januzaj na Chicharito yalisaidia sana kuleta uhai kwa timu hiyo na kuepuka janga la kufungwa nyumbani.

         
 

No comments:

Post a Comment