Azam imeweza kutumia udhaifu wa timu
ya Simba na kuweza kuwashinda kwa magoli 2-1, katika mchezo mzuri wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara uliochezwa katika uwanja wa taifa Dar es salaam.
Hadi kipindi cha kwanza
kinakwisha timu hizo zilikua zmefungana goli moja kwa moja.Simba ilikua ya
kwanza kupata bao lililofungwa na Ramadhani Singano baada ya kazi nzuri
iliyofanywa na kiungo wa kati wa Simba Said Ndemla kupiga pasi ya pembeni
iliyomkuta Zahor Pazi aliyempita
kirahisi beki wa kushoto wa Azam Wazir Seif na kupiga krosi ndogo iliyomkuta Singano aliyewahamisha mabeki wa Azam na
kupiga shuti lililopita kushoto mwa goli la Simba na kuandika goli la kwanza.
| ZAHORO PAZI AKIKIMBIA KUSHANGILIA BAADA YA KUTOA PASI YA GOLI LA KWANZA LA SIMBA |
Azam hawakutetereka na goli hilo kwani
walifanya shambulizi kubwa na pasi ndefu ya Abubakar Salum ilimkuta John Boko
aliyemzidi nguvu beki wa Simba Hassan Hatibu na kupiga shuti lililotoka nje.
Simba ilikua ikifanya mashambulizi
mengi kupitia kwa Singano ambae mara kwa mara alikua akimsumbua Said Morad na
dakika ya 34 alipiga pasi nzuri iliyomkuta Zahor Pazi aliyeingia nao
katika eneo la hatari na alippotaka kupiga aliwahiwa na Agrey Moris na kua kona
ambayo haikuzaa matunda.
| WACHEZAJI WA SIMBA WAKISHINGILIA GOLI LAO |
Azam walisawazisha kutokana na mpira
uliotoka katikati ya uwanja na Kipre Balou
alipiga pasi upande wa kulia mwa uwanja ukamkuta Abubakar aiyempigia pasi Erasto Nyoni ambae alimaliza uwanja na kupiga
pasi nzuri iliyomkta Kipre Tcheche aliyeukwamisha wavuni.
Kipindi cha pili Simba walifanya
mabadiliko kwa kumtoa Zahor Pazi na Amri
Kiemba na nafasi zao kuchukuliwa na Christopher Edward na Sino Augustino wakati
Azam walimtoa Said Morad na Josef Kimwaga na kuwaingiza David Mwantika na
Malick mabadiliko yaliyowasaidia sana Azam, kwani Mwantika aliweza kumzuia
Singano vizuri na kuziba njia zote za kupenyeza mipira.
| RAMADHANI SINGANO AKIJIPANGA KUMTOKA SAID MORAD |
Azam walipata bao la pili kupitia tena
kwa Kipre Tcheche aliyepigiwa pasi ndefu
na Abubakar Salum na kumpita kirahisi Wiliam Lucien na kuupiga mpira kiufundi
na kupita pembeni mwa lango la Simba na kuandika bao la pili.
Simba walipata nafasi ya kuswazisha goli
hilo baada ya Mombeki kumpigia pasi nzuri Sino lakini akashindwa kufunga.
| SINO AUGUSTINO,SURE BOY,MWANTIKA NA PEMBENI BALOU WAKIMPITA CHISTOFER EDWARD ALIYEUMIA |
Kwa ujumla
Simba hawakucheza vizuri kabsa katika mchezo wa huo kwani mabeki wake wa kati Owino na Hassan Hatibu walikua hawaelewani
mara kwa mara na hata Wiliam Lucien aliyecheza kama beki wa kulia alisumbuliwa
sana na Kipre Tcheche, hadi sasa timu ya Simba bado haijapata kikosi cha
kwanza na hilo linawasumbua sana.
| KOCHA WA AZAM AKIONGEA NA CAPTAI WA SIMBA KATIKA MECHI HIYO, OWINO |
Na hata mabadiliko
waliyofanya hayakuwasaidia sana lakini Azam walifanya mabadiliko na yalisaidia
kuongeza nguvu na ufundi hadi wakafanikiwa kupata ushindi.
No comments:
Post a Comment