Torres awamaliza man city
Fernando Torres ameweza kusaidia kutoa
pasi ya goli la kwanza na kufunga la pili na kuiwezesha timu yake ya Chelsea kuifunga
Man City kwa magoli 2-1.
Katika mchezo huo ambao ulikua mgumu na
kila mmoja akitarajia kuwa utaisha kwa sare ya goli 1-1 Torres alitumia vizuri
makosa yaliyofanywa na beki wa City Matija Natascic na kipa wake Joe Hart
kuchanganyana na mpira kumkuta Torres
aliyefunga kirahisi.
Aguero aliisawazishia City baada ya kupata pasi nzuri toka kwa Samir Nasri na akapiga mpira uliokwenda
pembeni mwa goli na kuandika goli.
Goli hilo liliwafanya Man City kuendelea kushambulia na Aguero alikosa
tena goli la wazi pale mabeki wa Chelsea walipodhani ameotea lakini alipojaribu
kuubetua mpira ukatoka nje. Na shuti kali la Ramirez aliyekua akihaha uwanja
mzima lilitoka nje idogo ya goli la City.
Gary Cayhil nusura aipatie timu yake goli lakini alipobaki na kipa wa City Joe Hart, aliupaisha mpira kwa mshangao wa wengi.
Torres aliyecheza vizuri sana katika mchezo
huo aliweza kuipa ushindi timu yake alipofunga dakika ya tisini ya mcezo na
kuifanya itoke uwanjani kwa ushind wa 2-1.
Kocha wa Chelsea alishindwa kujizuia kwa furaha na kukimbia had kwa masahbiki wa timu hiyo na kushangilia pamoja nao..





No comments:
Post a Comment