Tuesday, 29 October 2013

     mbeya city yashinda
   Mbeya derby
                                                 NA ABDUL SUDI,MBEYA

               Timu ya Mbeya City imefanikiwa kutoka na ushindi mnono wa magoli 2-0 dhidi ya wapinzani wao wakubwa timu ya  Tz Prisons  ya hapo hapo jijini Mbeya,  katika mchezo mkali uliojaa kila aina ya ufundi.
              Katika mchezo huo,  muamuzi Israel Mkongo toka Dar es salaam alimudu vilivyo na kusifiwa na mashabiki waliotazama mchezo huo.
ISRAEL MKONGO

                 Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko zilikua bado hazijafungana ingawa kosa kosa zilikua nyingi kwa kila timu.
KOCHA WA MBEYA CITY JUMA MWAMBUSI
       Prison ndio walioanza kutawala dakika za mwanzo kwani walifanya mashmbulizi mengi ingawa safu ya ulinzi ya Mbeya City iliyokua ikiongozwa na  Yusuph Abdallah na Deoratius Julius walifanya kazi nzuri ya kuwazuia washambuliaji wa Prison na hasa  Peter Michael aliyekua akiwasumbua mara kwa mara.
MBEYA CITY
                    Nao Mbeya City walizinduka na Alex Seth alifanya kazi nzuri mara kadhaa ya kuwatoka mabeki wa Tz Prisons na kupiga krosiambazo zilikkua zikiokolewa.
            Kipindi cha pili Prison walianza tena kwa kasi na kukosa goli la kuongoza baada ya kufanya shambulizi kali na mpira uliookolewa na mabeki wa Prison ulimkuta Peter Mapunda aliyepiga shuti kali na kuandika goli la kwanza.
TZ PRISONS
                 Mbeya City waliendelea kushambulia na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa kwa njia ya penati baada ya beki wa Prison kumfanyia madhambi shambuliaji wa Mbeya City Deus Kaseke,na Deogratus Julius akafunga penati hiyo.
WACHEZAJI WA MBEYA CITY WAKISHANGILIA GOLI LA KWANZA

                  Kwa kiasi kikubwa mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi ya kumbadilisha Jeremiah John aliyeumia na nafasi yake kuchukuliwa na Mwagane Yeya,na kkumtoa chipukizi Alex Seth na nafasi yake kuingia Peter Mapunda ndio yaliyobadilisha kabisa hali ya mchezo huo, kwani mashambulizi yaliongezeka na kufanikiwa kupata mabao yote mawili.

No comments:

Post a Comment