Saturday, 19 October 2013

 MAN UTD YABANWA TENA

Kwa mara nyingine timu ya Manchester united imeshindwa kupata ushindi nyumbani baada ya kulazimishwa sare na timu ya Southampton kwa kufungana goli 1-1.
    Suthampton walipata bao lao ikiwa imesalia dakika moja mpira kumalizika kwa goli lililofungwa na beki Dejan Lovren na kuzima ndoto za Man za kuondoka na ushindi.
             Man walikua wa kwanza kupata goli lililofugwa na RobinVan Persie baaada ya kazi nzuri iliyofanywa na kinda Adnan Januzaj  na kumpasia Rooney aliyepiga na kipa wa Southamton akashindwa kuuhiili na kumrudia Van Persie aliyeukwamisha wavuni.

   Van Persie tena nusura aipatie Man goli la pili lakini mpira aliopiga kichwa ukagonga nguzo.


     Baada ya mchezo kocha wa timu ya Southmpton Mauricio Pochettino alisema ameridhika na sare hiyo ingawa kulikua nafasi ya kuweza kushinda lakini kwa kupata sare ni jambo kubwa sana ukichukulia unacheza katika uwanja kama wa Old Traford. Nae kocha wa man David Moyes  alisema timu yake ilifanya kosa kuridhika na goli moja na hilo ndio tatizo kwani w
alipata nafasi wakashindwa kuzitumia hivyo wamestahili kupata hiyo sare.

No comments:

Post a Comment