USIOMBE KUKUTANA NA
MBEYA CITY,ni BALAA….
NA
ABDUL SUDI,MBEYA
wahamasishaji wa mbeya city
MBEYA CITY leo katika uwanja
wa kumbukumbu ya Sokoine imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga timu ya
JKT stars kwa goli 1-0 katika lig kuu ya
Vodacom Tanzania bara,huu ni mchezo wa nne mfululizo kwa timu hiyo kushinda
baada ya kuzifunga timu za Oljoro JKT 2-1,Rhino Rangers 3-1,kisha kuwafunga
Mgambo JKT 1-0 na sasa kuwafunga JKT Stars 1-0.
Goli la ushindi kwa Mbeya City
lililofungwa na mshambuliaji wake hatari Jeremiah John katika dakika ya 30 ya
mchezo baada ya kona iliyookolewa na walinzi wa JKT na mpira kumkuta mfungaji
aliyepiga shuti kali lililotinga wavuni.
Mbeya City itajilaumu kwa kukosa
magoli mengi ya wazi hasa kipindi cha pili kwani waliutawala mno mchezo na
kushinda golini mwa JKT lakini uhodar wa kipa na kutokua makini kwa
washambuliaji wake kuliifanya timu hiyo kumaliza mchezo na goli hilo hilo moja,
Kocha wa timu hiyo Juma Mwambusi kama kawaida aliwashukuru sana mashabiki wa
timu hiyo kwa kuwapa sapoti kubwa na pia aliwashukuru wachezaji wake kwa kujituma
na kuweza kufanikisha ushindi huo.
Kwa ushindi huo timu ya Mbeya City imefikisha
pointi 20 sawa na Azam na kuongoza ligi
hiyo kwa muda.
KIVYETU VYETU
Na katika mchezo mwingine wa
ligi hiyo,timu ya Mtibwa imeifunga Mgambo
JKT kwa magoli 4-1 mchezo uliochezwa
katika uwanja wa manungu.magoli ya Mtibwa yalifungwa na Shaaban Nditi aliyeunganisha
kwa kichwa kona ya Awadh Juma ,na goli la pili lilifungwa na mchezaji
chipukizi Juma Luzio baada ya kupata
pasi ya shaaban nditi,na goli la tatu lilifungwa tena na Juma Luzio baada ya kupata mpira katikati ya uwanja na
kuwapita mabeki wa mgambo kisha akakimbia
na kupiga shuti kali la mguu wa kushoto
lililomshinda kipa wa Mgambo Kaviche na
kuingia.Goli la nne lilifungwa na Shaaban Mkopi.Mgambo walikuja kupata goli la kufutia
machozi kupitia kwa Nguya dakika ya 83 kwa njia ya penati baada ya
mshambuliaji wake kuangushwa katika eneo la hatari.
Nayo timu ya Kagera Sugar imefanikiwa kuifunga timu ya Coastal
Union ya Tanga kwa goli moja lililofungwa na Salum Kanon kanon dakika
ya 60 kwa njia ya penati.
Azam wameifunga JKT Oljoro ya
Arusha goli moja liliofungwa na kiungo
wake Mcha Khamis katika dakika ya 67.
Nayo Ashanti imelazimisha sare ya magoli 2-2
na timu ya Ruvu Shooting katika mchezo uliochezwa uwanja wa AZAM,Ruvu ilikua ya
kwanza kupata magoli yake yote mawili moja kila kipindi yaliyofungwa na lakini
Ashanti walikuja kuzinduka dakika 20 za mwsho na kufanikiwa kusawaziha magoli
yote mawili.


No comments:
Post a Comment