Simba
Ilivyo chomoa
kwa
yanga
NA ABDUL SUDI.
![]() |
| KIKOSI CHA SIMBA |
Wakati wa mapumziko,kila shabiki wa mpira
Tanzania,iwe anatazama akiwa uwanjani au katika televisheni,au awe anasikiliza
katika radio aliamini kabisa Yanga wameshashinda mchezo huo,kilichokua kikisubiriwa
ni idadi ya magoli yatakayoongezeka kipindi cha pili.kwani pamoja na kuongoza
kwa magoli matatu walikuwa wameutawala mchezo katika idara zote,katikati
Athumani Iddi,Frank Domayo na Haruna Niyonzima walikua wamepashika
vilivyo.Mrisho Ngasa na Didier Kavumbagu walikua wanasumbua sana,na Hamisi
Kiiza alikua akirudi kuwasaidia viungo na kuipeleka mipira mbele na kwa kasi
waliyoku nayo Yanga,mchezo ulionekana tayari umekwisha.
![]() |
| KIKOSI CHA YANGA |
Lakini sio kwa Kibaden na msaidizi wake
Jamhuri Kihwelo,wao walikua na imani kua mambo yanaweza kubadilika,walitulia
wakatazama nini tatizo,wakaona wametawaliwa katikati wakaamua kufanya
mabadiliko yaliokua na manufaa makubwa katika mchezo huo,wakamtoa Chanongo
ambae hakucheza katika kile kiwango alichozoeleka,wakamtoa na Humud ambae kwa
vile alichezeshwa nafasi ambayo hakuizoea ya kiungo wa mbele, ilikua inamuwia
ngumu sana kugawa mipira,alikua anakaba vizuri lakini anapotoa pasi alikua mara
nyingi anawapasia maadui hivyo kufanya Jonas Mkude aliyecheza kiungo wa chini awe
na kazi ngumu sana ya kuitafuta mipira iliyoharibika.
Wakawaingiza watoto Wiliam Lucian,na Said
Ndemla ambao kwa kiasi kikubwa ndio waliobadili sura ya mchezo.walisaidiana
kukaba na kugawa mipira vizuri sana na kumfanya Mkude awe na sehemu kubwa sana
ya kucheza katikati,na kutokana na kuchoka kwa Athumani Iddi Simba walitawala
mno kiungo katika kipindi cha pili.na wakatengenza nafasi nyingi za kufunga na
wakafanikiwa kuzitumia tatu kati ya hizo.
Hawakuachia hapo kwani waliendelea
kushambulia na kufanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Hamisi Kiiza baada ya
mabeki wa Simba kushindwa kuuzuia mpira uliorushwa na Mbuyu Twite na kumkuta
Kiiza aliyeusukumiza wavuni.Simba wakapoteana na Yanga wakazidi kucheza kwa
uhakika,Chanongo akawa anashindwa kumsaidia Haruna Shamte ambae muda mwingi
alijikuta anaingia katikati kwenda kuwasaidia mabeki na viungo hivyo pembeni
Ngasa akawa huru sana,Athumani Iddi akawa anapiga pasi pembe zote na Niyonzima
akasogea sana katikati na kuwafanya viungo wa Simba kushindwa kuhimili nguvu
kubwa ya Yanga.
![]() |
| MOMBEKI AKIWAHI KUANZISHA MPIRA BAADA YA GOLI LA PILI LILILOFUNGWA NA OWINO |
Wachezaji wa Yanga wakaona
wamemaliza mchezo wakawa wanacheza kwa mbwembwe
na hasa Mrisho Ngasa na Nadir Haroub,wakawa wanaucezea mpira wanavyotaka,hawakujua kua
wanawapa Simba nafuu kwani tayari walikua wamepoteana.
Hadi mapumziko
Yanga wakawa wanaongoza kwa magoli matatu kwa bila.
Kipindi cha pili Simba
walifanya mabadiliko baada ya kuwatoa Humud na Chanongo n nafasi zao
kuchukuliwa na Said Ndemla na Wiliam Lucien ambao wakaubadilisha mchezo kwa
kila hali.Wakamsaidia Mkude kukaba katikati na kuvuruga mipango ya Yanga,na kwa
vile Athumani Iddi alikua tayari kachoka akawa anacheza nyuma sana hivyo
kuwafanya viungo wa Simba kummeza Domayo,na Niyonzima akawa hapati tena mipira
toka katikati.wakafanikiwa kupata bao la kwanza kupitia kwa Betram Mombeki
aliyepata pasi nzuri toka kwa Hamis Tambwe aliyekimbia na mpira hadi pembeni
mwa lango la Yanga na kupiga pasi
iliyomkuta Mombeki na akaupiga kiufundi na kuandika bao la kwanza.
![]() |
| KELVIN YONDANI AKIWA HAAMINI |
Goli la pili lilitokana na kona upande huo
huo wa kulia na Ramadhani Singano alipopiga hiyo kona ilimkuta Josef Owino
aliyepiga kichwa na kuandika goli la pili.Yanga wakaamua kumtoa Kiiza na nafasi
yake kuchukuliwa na Simon Msuva,mabadiliko yaliyowamaliza kabisa nguvu Yanga
kwani hawakuwa tena na mipango ya kushambulia.Msuva na Ngasa wote wakawa
wanacheza upande wa kulia na Niyonzima akawa kaingia sana katikati hivyo pembeni
upande mmoja kwa Yanga hakukua tena na
mtu,Simba wakawa wamekamata kabisa katikati.
Ngasa alipata nafasi ya kumaliza mchezo
baada ya kuwatoka mabeki wawili wa Simba lakini uhodari wa kipa wa Simba Abel
Dhaira ulimkosesha goli kwani aliokoa ikawa kona ambayo haikuzaa matunda.
![]() |
| GILBERT KAZE |
Simba
walipata bao lao la tatu kupitia kwa beki
wake wa kati Gilbert Kaze baada
ya faulo iliyotokea upande ule ule wa kulia ikapigwa na Nassor Cholo na kumkuta
Kaze akiwa hana mtu wa kumkaba kwani mabeki wawili wa Yanga walikua wamemkaba
Mombeki na hivyo Kaze akapiga kichwa na kuandika bao la tatu.
![]() |
| WACHEZAJI WA YANGA WAKILAUMIANA BAADA YA KUINGIA GOLI LA TATU |







No comments:
Post a Comment