Real yatota kwa barca
Magoli yaliyofungwa na Neymar na
Alexis yaliwafanya Barcelona kutoka na
ushindi mzuri wa magoli 2-1 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Real Madrid.
Barcelona walikua wa kwanza kupata
bao katika dakika ya 19 lililofungwa na Neymar baada ya kupokea pasi toka kwa
Andres Iniesta.
Real walishambulia sana ii kupata bao la
kusawazisha lakini kipa wa Barcelona alikua imara na kuzuia micho ya Khedira na
Ronaldo waliokuwa na uchu wa kufunga.
Real waliendelea kushambulia na Ronaldo
alingushwa katika box la penati lakini mwamuzi hakutoa penati na baadae Benzema
alipiga shuti likagonga mwamba.
Zikiwa zimesalia daika 12
mpira kumalizika Barcelona walipata bao
lililofungwa na Alexis Sanchez na kumaliza kabisa matumaini ya Real
kusawazisha.
Goli la kufutia machozi la Real
lilipatikana katika dakika za nyongeza likifungwa na Jesse baada ya kupokea
mpira toka kwa Ronaldo.
Kiungo Gareth Bale hakuonyesha makeke yake zaidi ya
kupiga shuti kali lililotoka nje na baadae kupewa kadi ya njano kwa mchezo
mbaya. Alitolewa katika dakika ya 60 na
nafasi yake ikachukuliwa na Karim Benzama aliyeongeza uhai katika timu yake.





No comments:
Post a Comment