MBEYACITY YAICHAPA OLJORO 2-1
mbeya city
Timu ya Mbeya
City imefanikiwa kuifunga timu ya JKT Oljoro ya Arusha kwa magoli mawili kwa
moja katika mchezo mkali na mzuri uliochezwa katika uwanja wa sheikh Amri Abeid
Arusha.City ndio waliokuwa wa kwanza kupata
bao lililofungwa na mshambuliaji hatari Mwagane Yeya baaada ya krosi safi
iliyopigwa toka kushoto mwa uwanja na mpira ukamkuta Paul Nonga aliyepiga shuti
kali lililomshinda kipa wa Oljoro na mpira ukawa unaelekea golini na ndipo mwagane akaumalizia na kuandika goli
la kwanza.City walikitawala kipindi cha kwanza na hadi mapumziko goli likawa
hilo moja.kipindi cha pili Oljoro waliingia kwa nguvu na kufanya mashambulizi
mengi kuelekea kwa City,na uhodari wa mabeki wa City wakiongozwa na Yohana
Morris na kipa Baruan walikua makini na kuweza kkuzuia mashambulizi hayo.City
wallipata bao la pili kwa counter attack baada ya Oljoro kufanya shambulizi
kali golini mwa City na ndipo kipa wa City Baruan alipodaka akapiga mpira mrefu
uiomkuta Peter Mapunda aliyekua katikati ya mabeki wawili na kufanikiwa
kuwapita na kukimbia mbele kidogo na kupiga shuti kali lililomshinda kia wa
Oljoro na kuandika goli la pili.ni moja kati ya magoli mazuri sana yaliyofungwa
katika ligi ya mwaka huu.Oljoro walipata goli lao kipindi ch pili baada ya
kufanya mashambulizi mengi na kufanikiwa kupata bao hilo,hadi mwisho JKT Oljoro
1 na Mbeya City 2 WELL DONE MBEYA CITY
No comments:
Post a Comment