Mbeya city uso kwa uso na jkt ruvu
NA ABDUL SUDI
SHABIKI WA MBEYA CITY
Timu ya
Mbeya city iliyo katika form kali,jumamosi inapambana naJKT ruvu katika
mfululizo wa michezo ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania.Katika michezo yake iliyopita
Ruvu stars ilifungwa magoli 3-0 na Azam na kabla ya hapo walikua wamefungwa naSimba2-0,kisha
na Mtibwa 2-1 hivyo watakua wanatafuta kwa nguvu sana ushindi ili uweza
kujiweka katika nafasi nzuri.
Mbeya city wana kumbukumbu
nzuri ya ushindi mfululizo katika michezo yake kwani katika michezo mitatu iliyocheza
ugenini imefanikiwa kujipatiapoint zote
tisa kwakuwafunga JKT Oljoro 2-1mjini Arusha,kisha wakawafunga Rhino yaTabora
3-1na mwisho wamewafunga Mgambo JKT
kwagoli 1-0.Hivyo wako ktika kiwango kizuri na ukichukulia wanacheza katika
uwanaja wao wa nyumbani ulio na sifa ya kujaza mashabiki wake wanaoisapoti timu
hiyo kwa kuishangilia mwanzo hadi mwisho.
Akielezea mchezo huo,kocha wa
timu ya Mbeaya City Juma Mwambusi amesema wanauchukulia kwa tahadhari kubwa
sana mchezo huo kwani kwa vile wameshashinda mechi tatu mfululizo wanajua wapinzani wao watakua
wamejipanga vilivyo kujilinda na kufanya
mashambulizi ya kushtukiza,hivyo amewaambia vijana wake watashambulia mwanzo
hadi mwisho ili wawezekuondoka na point tatu muhimu katika mchezo huo,aliongeza
hadi sasa timu iko vizuri na hakuna majeruhi wa kutisha katika timu hiyo,hivyo
wapenzi na mashabiki wa soka jijini hapa wategemee mchezo mzuri na Insha allah
timu itashinda.
Michezo mingine inayotarajiwa kuchezwa
mwisho wa wiki hii ni Kagera sugar watawakaribisha
Coastal Union,JKT Oljoro watacheza
Azam,wakati Mtibwa sugar watakua wenyeji wa Mgambo shooting,na Ashanti
watacheza na Ruvu Shooting.jumapili ni Simbana Yanga.

No comments:
Post a Comment