OZIL
Atabiriwa kuwapa
arsenal
ubingwa
Kiungo wa
timu ya Arsenal Saint Carzola anaamini ujio wa mtaalam Mersut Ozil katika klabu
hiyo umewapa hamasa wachezai wengine kupigania ubingwa na kumaliza ukame wa
makombe.
Kocha wa Arsenal,Arsene Wenger
alivunja rekodi za gharama za usajili wa timu hiyo baada ya kumchukua Ozil
kutoka Real Madrid dakika za mwisho za dirisha dogo la usajili ka gharama ya
paundi milioni 42.
Carzola anasema bado anashangaa kwa
nini Real Madrid walimuachia mchezaji mwenye kiwango bora kama cha Ozil na
alifurahi sana kumuona akijiunga na Arsenal.
“nilishangaa sana kusikia Madrid wanamuacha na nilifurahia mno kuona mchezaji
mwenye kiwango kama chake anakuja kucheza na sisi,na alipokuja hakua na makeke
yoyote,alikuja na kuanza kufaya kazi mara moja,ni mchezaji ambae unajifunza
mengi sana toka kwake,na ni mtaalamu sana”alisema Carzola.
Akimuongelea Ozil mshambuliaji wa
zamani wa timu hiyo Robert Pires amesema “Ozil ameleta kitu ambacho kilikua
kinahitajika muda mrefu sana,Arsenal wamezoeleka kwa kukaa sana na mipira
lakini hawako makini kwa kutoa pasi za mwisho lakini sasa amekuja Ozil
anaifanya hiyo kazi na kuwarahisishia wengine kufunga kirahsi,hadi sasa tayari
kafunga na kutoa pasi tatu za magoli,ni kiwango kizuri sana
Kocha Arsene Wenger yeye anasema kuja kwa Ozil kumeamsha ari kwa wachezaji
wengine wa Arsenal,ni usajili sahihi ambao malio yake yankuja pale pale bil
kusubiri muda.
Ozil alicheza michezo 105 akiwa Werder Bremen na kufunga magoli 16 n kutoa pasi za mwisho 55,alipokwenda Real Madrid alifunga magoli 27 akatoa pasi 81 katika michezo 159 na kumfanya awe ni kiungo mshambuliaji bora katika ligi zote za ulaya kwa msimu uliopita.na wengi wanaamini alikua ni kiungo mshambuliaji bora duniani msimu uliopita.




No comments:
Post a Comment