Friday, 1 November 2013

Yanga yanoga

       Timu ya Yanga imeweza kuwafunga Ruvu JKT kwa magoli 4-0 katika mchezo wa upande mmoja ambapo Yanga waliutawala mchezo huo katika vipindi vyote viwili.
     Yanga walipata goli la kwanza mapema katika kipindi cha kwanza  lililofungwa na Mrisho Ngasa baada ya kupata pasi toka kwa Domayo  na akawahadaa mabeki wa Yanga  wakidhani anataka kutoa pasi  ndipo alipopiga shuti kali lililomshinda kipa wa JKT  na kuingia golini.
      JKT hawakuonyesha kutulia na mabeki wake walikua kila mara wakijichanganya na kuwafanya Yanga wazidi kutawala mchezo, goli la pili lilifungwa tena na Mrisho Ngasa baada ya mpira uliorushwa na Mbuyu Twite kuwapita mabeki wa JKT na ukadunda na kumkuta Ngasa aliyepiga kichwa na kuandika goli la pili.
      JKT walicheza bila ya maelewano na hasa viungo wao waliokua wakipoteza mipira mara kwa mara na kuwafanya viungo wa Yanga kua na kazi rahisi ya kusambaza mipira kila upande.
   Yanga walipata goli la tatu kupitia kwa beki wake wa kushoto Oscar Joshua baada ya kona iliyopigwa na Ngasa kuokolewa kizembe na mabeki wa JKT na mpira kumkuta Joshua aliyepiga shuti zuri la mguu wa kushoto na kuandika goli la tatu

      Waliendelea kushambulia na mshambuliaji wake Jerry Tegete alikosa nafasi tatu za wazi kufunga magoli na baadae kufanikiwa kufunga baada ya kuukuta mpira uliowapita mabeki wa JKT na kuandika goli la nne.hadi mpira unamalizika Yanga wakaondoka na ushindi wa magoli manne kwa bila. 

No comments:

Post a Comment