OSCAR… kiungo
chelsea
NI mzuri sana kwa kupiga
shuti akitumia pembeni mwa mguu (outer),
anapiga chenga za haraka sana bila kufikiria kwa muda mrefu, na anajua ni muda gani apige shuti hata akiwa
mbali na goli,mara nyingi anafanikiwa kupata magoli na yanakua mazuri sana.
Wengi walikua wakimfananisha na Kaka kwa jinsi anavyomudu kugawa mipira akiwa
kama kiungo wa juu, lakini ameonyesha
ana uwezo hata wa kua mshambuliaji kani mara nyingi mpira unapofika katika
penat box nae tayari anakua kafika.
Oscar alizaliwa mwaka 1991 na alianza kucheza mpira katika timu ya Sao
Paolo mwaka 2008, lakini mwaka 2009 aliipeleka mahakamani timu hiyo baada ya
kukiuka makubaliano ya mkataba waliokuwa wameweka. Baada ya hapo alihamia timu
ya Internacional alikokaa miaka mitatu hadi alipohamia Chelsea.
Akiongelea kipajichake anasema ni
kitu alichokirithi toka kwa baba yake ambae ingawa alikua na kiwango kikubwa
sana lakini mazingira yalimzuia kufika mbali zaidi na pia mjombake ambae nae
kama baba yake hakufika mbali ingawa alikua na kipaji.Baba yake alifariki Oscar
akiwa na miaka mitatu hivyo hakuweza kumuona mwanae akiwa ni mmoja a nyota wa
soka duniani.
“ingawa baba yangu hayupo
duniani lakini nina furaha kwamba angalau mjomba yupo na anafatilia sana
maendeleo yangu kwani kila nikicheza mechi lazima niikute message zake katika
simu akinipongeza na kunikosoa kwa kila ninalofanya uwanjani,hua nazisubiri kwa
hamu message zake na za binamu zangu,hua zinanipa faraja sana na kuiona
nawakilisha familia duniani”alinukuliwa Oscar. “natamani sana kama bba yangu
angekuwepo,lakini ndio hali ya dunia,huwezi kuhindana nayo,kilichopo ni kua
nafanya vizuri na malengo aliyokua nayo wakati kijana mimi nayatimiza,na
ninajitahidi sana kufika mbali zaidya hapa”alisema Oscar.
Kwa sasa Oscar amekua
ni tegemeo la timu ya Chelsea kwani mara nyingi anacheza kama kiungo wa
mbele,anagawa mipira na anafunga magoli muhimu kila akipata nafasi.





No comments:
Post a Comment