PRODUCER EPHRAIM KAMETA 
Wengi
wamemjua Ephraim Kameta baada ya kumtoa msanii maarufu sana wa bongo
flava, Mr nice lakini Kameta hakuanza leo kufanya
shughuli za muziki, kwani wakati bado mdogo kabisa mwaka 1984 alikua akipiga na
wakongwe kama marehemu Patric Balisidya na Ludala katika bendi iliyokua
ikijulikana kama African Roots,na hata katika ule mwimbo maarufu sana wa bendi
hiyo wa JIRANI, Kameta ndie aliyepiga lead guitar. “nilifurahia sana kufanya kazi pamoja na mtu
kama Patric Balisidya kwani uzoefu wake tu katika muziki ni shule tosha,maana
alikua anajua sana muziki.”
 |
| KAMETA AKIWA NA TUZO ZAKE |
Kameta alizaliwa mkoani Mbeya eneo la soko
matola na kupata elimu yake mkoani humo
humo akianzia na elimu ya msingi katika shule ya Majengo na kumalizia katika
shule ya mbeya primary ambayo kwa sasa ipo shule ya Meta. Alijifunza kupiga muziki kanisani, kanisa la ASSEMBLIES OF GOD ambalo baba yake alikua ni mchungaji na walikua wakiishi jirani na hilo kanisa, alianza
kugusa chombo kimoja kimoja na matokeo yake akaja kuwa mtaalamu wa kupiga kila
aina ya zana. “Nilipopata tu urefu wa kukaa katika kiti na
kuifikia organ,nikaanza kujifunza kupiga organ,
baadae akaja mpiga gita mmoja akiitwa John, nikatokea kuhusudu sana upigaji
wake, nae akanisogeza na kuanza kunifundisha kupiga gita, na kuna wakati yalikuja mahubiri makubwa pale
kanisani na siku hiyo watu wakamshangilia sana mpiga gita la besi hapo
nikatamani sana na mimi niwe mpiga besi,nikamfata nae hakua mchoyo akanifundisha…matokeo
yake ikawa kila akichelewa mpigaji wa chombo chochote naitwa na kuziba nafasi
yake,na sikuwaangusha kwani nilikua napiga vizuri kiasi hakuna aliyewahi
kugundua kama mimi si mpigai rasmi” alinisimulia
huku akicheka.
Mwaka 1984 akahamia Dar, na huko
ndipo akakut
 |
| AKIWA NA FAMILIA |
ana na wataalamu kama kina Patric Balisidya na bendi ya African
Roots na kurekodi nao nyimbo kadhaa kisha akarudi tena Mbeya, akajiunga na bendi ya MIONZI ambako alikutana
na wanamuziki maarufu wakati huo kina Martin aliyekua akipiga kinanda na mdogo
wake Deric aliyekua akiimba, pia walikuwepo kina Noel. Lakini baadae mwaka 1994 akarudi tena Dar na
kujiunga na bendi ya INAFRICA akiwa na kina ras Pompi pamoja na Enrico. Na hapo
pia alirikodi nyimbo kadhaa kabla hajaenda kuanzisha bendi ya OLDUVAI akiwa na
kina Noel na Issa na hapo walifanikiwa kurekodi nyimbo nyingi lakini mojawapo
iliyokua maarufu zaidi ni ‘baba kaleta panya’
“Mwaka 1999 nilipata nafasi ya kwenda
Germany katika kozi ya muziki,na nilisoma kwa mwaka mmoja na kupata diploma ya
kutayarisha muziki na niliporudi mwaka 2000 ndio nikaamua kuanzisha kampuni yangu ya production ya AK PRODUCTION,”alisema
Kameta “Nilipoanza production nikapata
watu kadhaa wa kuwatengenezea nyimbo zao,na ukweli zilikua zinafanya vizuri
sana, kuna muda nilifanya kazi na watu
ambao hata hawajawahi kufikiria kua siku moja watakua wanamuziki,na kazi zao
nilipomaliza zikawa nzuri kiasi hata wenyewe walishangaa walipozisikia mara ya
kwanza,Mtu kama Bambo alipokuja na wazo lake la kutoa mwimbo wa KITAMBI,hakuna
aliyedhani kama utakua mzuri,lakini tukakaa chini na kuufanyia kazi matokeo
yake wote mmeona, hata King’wendu nae
tulifanya nae kazi ya kuutengeneza mwimbo wa MAPEPE, ingawa inakua ngumu sana kufanya nao kazi, lakini
ukidhamiria inalipa,nao ukaja kua ni hit sana,kila mtoto anaujua MAPEPE….”
 |
| FAMILIA |
Akiongelea kuhusu kazi ambazo aliumiza
sana kichwa kuzitengeneza,KAMETA ambae sasa hivi ana kampuni inayoitwa TIKA
PRODUCTION hakosi kukuambia kuhusu albam mbili aliomfanyia MR NICE “Unajua mwaka 2001/02 mimi ndie nilimfanya
mr nice atoke, sababu albam zake zote
mbili nilitoa mimi,na nilikua naumiza sana kichwa, sio siri MR NICE ni mzuri sana wa kuimba
lakini inatakiwa uujue sana muziki ili umfanyie kazi zake, kwangu mimi nasema,hata leo MR NICE akija
kwangu, atarudi kule kule juu alikokua, sababu mimi ni mwanamuziki na najua
anachohitaji, najua mapungufu yake na
pia tayari tulikwishajuana , hivyo ni rahisi sana kumtengenezea kazi na ikamtoa
tena” alipoulizwa kwa nini walitengana kikazi na MR NICE alinijibu
kifupi sana “alipopata mafanikio akapata pia na washauri
wabaya, hivyo tukashindana, na hilo limetokea si kwake tu bali kwa wanamuziki
wengi, unaumiza kichwa kwa kumuona ana
talent lakini akitoa mwimbo mmoja tu na
kua hit, anakimbilia kwa maproducer wao waliojifunza kutengeneza muziki kwa
computer, baadae ana flop anaanza kuhangaika,
wapo wengi sana wa aina hiyo”
 |
| STUDIO |
Kameta kawatoa watu wengi sana.wanamuziki
kama MEZ B na mwimbo wake wa KIKUKU mwaka 2002,
wakati mwaka 2003 akamtoa SUPER DANGER na hit yake ya UTANIKUMBUKA, pia mwaka 2004 akamtoa RICHIE RICH na mwimbo
wa FUNGUO.. wote hao alifanya nao kazi
zilizokuja kua hit sana kwa miaka hiyo. Hata
wanaoimba nyimbo za dini pia kafanya Kazi na wasanii wengi sana maana mwaka
2005 alifanya kazi na BIG NOVEMBER CRUSADE na wakatoa mwimbo wa SIPATI
PICHA, akafanya na mwanamuziki maarufu
sana hapa Tanzania, BONIFACE MWAITEGE
wakatoa mwimbo ambao hadi leo bado ni hit wa UTANITAMBUAJE KAMA NIMEOKOKA, akaja kumtengenezea tena mwanamuziki AMBWENE
mwimbo wake wa MAJARIBU NI MTAJI, pia NEEMA MWAIPOPO na mwimbo wake wa RAHA JIPE
MWENYEWE pia aliufanya KAMETA.baadae akaja kumtengenezea BONY mwimbo wa
MAMA,kisha msanii machachari sana wa nyimbo za kwaya JOSEF NYUKI nae alikuja na
kufanya nae kazi na wakatoa nyimbo yake ya TEGEMEO LANGU, na tena akafanya kazi
na BAHATI BUKUKU na kumtengenezea mwimbo wake wa NIMESAMEHEWA DHAMBI SIO
MAJARIBU…kisha akaja NESTA SANGA wakafanya UWAHONGERE,na hata ENOCK nae pia
walifanya nae kazi katika mwimbo wa ZUNGUKA ZUNGUKA . Hivi sasa Kameta
anamializia kazi ya msanii mwingine aitwae PIUS BUTOKE ambayo nayo anaamini
itakua hit sana.
 |
| MTAMBONI |
Mwisho wa mazungumzo yake alisema “natamani sana kufanya kazi na wasanii wa
Mbeya,maana najua na kuamini kuna talent nying sana ziko Mbeya,nikifananisha na
watu ninaofanya nao kazi,watoto wa Mbeya wako juu sana,sijui tatizo linakua
nini,lakini kama wakitaka msaada toka kwangu nawakaribisha sana tuje tufanye
nao kazi”alimalizia KAMETA.
No comments:
Post a Comment