Sunday, 13 October 2013

mbeya city......MADE IN MBEYA……..

                            na abdul sudi.

                Timu ya soka ya Mbeta City imefanikiwa kuendeleza wimbi la ushindi ugenini baada ya kuifunga timu ya Mgambo shooting kwa goli moja kwa bila,kabla ya mchezo huo Mbeya City iliwafunga  Oljoro JKT ya Arusha 2-1,ikawafunga tena Rhino ya tabora kwa magoli 3-1 na leo tena imewafunga Mgambo shooting goli moja bila.katika mchezo wa leo goli la Mbeya City lilipatikana katika kipindi cha kwanza likifungwa na mshambuliaji wake hatari Jeremiah Juma.kpindi cha pili Mgambo walijitahidi kulishambulia lango la Mbey a City ili upta bao la kusawazisha lakini uhodari wa ngome ya City uliwanyima nafasi ya kumfikia kipa wao.Akiongea baada ya mchezo kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi alisema anashukuru vijana wake wamepigana na kufanikiwa kupata point zote tatu na sasa hvi anatazama mchezo ujao ambapo watacheza nyummbani na timu ya JKT Ruvu.aliwashukuru mashabiki wa soka wa moa wa Mbeya waliosafiri kuifata timu yao na kuwaahidi vijana wake watafanya kila wawezalo ili kuzidi kufanikiwa.

Mbeya City inatarajia kucheza na Ruvu JKT tarehe 19  mwezi huu jijini Mbeya na tarehe 26 mwezi huu watakua na kazi nzito ya kukutana na ndugu zao wa TZ Prisons katika mechi inayotaraiwa kuvutia maelfu ya wakaziwa jiji la Mbeya.

1 comment:

  1. Mechi ya Tz. Prison na Mbeya city itakuwa na ushindani wa hali ya juu sana, hasa ukizingatia kwamba kiwango walichoonyesha Mbeya city ni cha kushangaza kutokana kwanza na ugeni wa timu yenyewe katika mashindano haya makubwa kabisa kwa ligi ya nyumbani, na kwa upande wa Tanznia Prison wameonyesha kiwango kizuri japo matokeo hayakuwa upande wao kwa kiasi fulani, naamini watapigana ili kujiweka katika mazingira mazuri katika msimamo wa ligi na pia kulinda heshima yao mbele ya timu hii ngeni lakini hatari sana katika ligi.

    ReplyDelete